Wilaya ya kilwa ina takribani hekata 14,212 ambazo zipo kwaajili ya kufanya uwekezaji wa viwanda vikubwa na viwanda vya kati. Kuna viwanda vidogo vidogo vinavyo zalisha bidhaa hasa samani za majumbani ambazo hutengenezwa kwa ujuzi mdogo na kwa teknolojia duni, pia kuna viwanda vidogo vya kukausha samaki ambavyo vipo eneo la Kivinje na Somanga, viwanda vidogo vya kutengeneza na kufunga chumvi ambavyo vipo katika maeneo ya mashamba ya chumvi yaliyopo Kilwa Masoko na maeneo ya Kata ya Tingi, Miteja na Somanga.
Hivyo Halmashari ya Wilaya ya Kilwa inawakaribisha wawekezaji kuja na kuwekeza katika Viwanda vya kati na vikubwa kwakuwa miundombinu iliyopo inaruhusu hasa upatikanaji wa umeme wa uhakika, barabara na rasilimali watu ambavyo ni muhimu katika uwekezaji wa viwanda, uwepo wa malighafi hasa za gasi ambayo ni muhimu kwa kutengeneza saruji, uwepo wa maji ya chumvi, uwepo wa madini ya Nitrous(vilipuzi), uwepo wa Samaki wengi na Dagaa wanaopatikana katika Bahari ya Hindi.
Wawekezaji wanakaribishwa kuja na kuwekeza katika Sekta ya Viwanda katika maeneo yafuatayo;
A. Viwanda vya Saruji
B. Kiwanda cha kuchimba na kuchakata Gesi
C. Viwanda vya kutengeneza vilipuzi
D. Viwanda vya kutengeneza na kufunga Chumvi
E. Viwanda vya Kuchakata Samaki
F. Kiwanda cha Mbolea
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa