Watumishi wa timu ya Simba wameibuka na ushindi wa mabao 5–3 dhidi ya watumishi wenzao wa timu ya Yanga katika mchezo wa kirafiki uliochezwa tarehe 4 Septemba 2025 katika uwanja wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa.
Mchezo huo umehusisha watumishi kutoka taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, ukiwa na lengo la kuimarisha afya, kujenga mshikamano kazini, na kuhamasisha ushiriki wa watumishi katika michezo kama sehemu ya burudani na mazoezi ya mwili.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Afisa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Wilaya ya Kilwa, Bi. Veneranda Maro, amewapongeza washiriki wote kwa kujitokeza kwa wingi na kuonyesha nidhamu, umoja na ushindani wa kiurafiki.
“Michezo ni nyenzo muhimu katika kuimarisha afya, kujenga undugu na kuongeza ari ya kufanya kazi kwa bidii. Ni matumaini yangu kuwa ushiriki huu utaendelea kuwa chachu ya mshikamano na utendaji bora mahali pa kazi,” amesema Bi. Veneranda
Aidha, Bi. Veneranda amesema kuwa Ofisi ya Utamaduni, Sanaa na Michezo itaendelea kuunga mkono jitihada za kuendeleza michezo na kuhamasisha ushiriki wake katika ngazi mbalimbali za wilaya.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa