Kilwa ina maeneo mazuri ya kitalii yenye ikolojia nzuri, makumbusho pamoja na maeneo ya wanyama wa mwituni. Maeneo haya yamekuwepo kwa takribani miaka mingi iliyopita lakini hayajaendelezwa vizuri kwa kuboresha miundombinu ya kuweza kuwavutia watalii wandani na watalii wa nje. Katika wilaya ya kilwa kuna maeneo ya fuatayo ambayo ni muhimu kwa shughuli za kitalii ambayo yanavivutio vya asili, Magofu ya kale yaliyopo Kilwa kisiwani na kilwa kivinje, mapango ya Nandete yaliyopo katika kata ya Kipatimu, makaburi ya watu wakale hasa kipindi cha biashara ya utumwa yaliyopo Kilwa Kisiwani.
Vivutio vingine ni viboko waliopo mto Nyange, Misitu ya asili ambayo ina ndege wazuri na wakuvutia na fukwe nzuri zilizopo mwambao wa bahari ya Hindi.
Hivyo uwepo wa vivutio hivi unafanya kuwepo kwa hekta 844.24 ambazo zinaweza tumika kwa fursa za uwekezaji katika maeneo yafuatayo; hotel za kitalii, nyumba za kulala wageni wanotembelea vivutio vya kitalii, maeneo ya michezo kama mabwawa ya kuogelea na sehemu za kucheza watoto, kuwekeza katika usafiri wa maji kwakutumia boti ziendazo kasi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa