Kuhakikisha uwazi wa taratibu, miundo na mawasiliano
Masula ya kifedha yanawekwa wazi kwa wananchi wote na wadau wengine
Shughuli zote za kifedha zinafanyiwa kwa ukaguzi na uchunguzi
Shughuli za Halmashauri ya Wilaya zinapaswa kuzingatia kuleta matokeo katika jamii.
Jamii inapaswa kuruhusiwa kufuatilia na kutathmini matokeo ya Halmashauri katika ngazi za mitaa
Kila mtu anapaswa kuwajibika kwa maamuzi na matendo yake
Kutumia muda na Nguvu katika kuhakikisha kuwa wananchi/watu wanapata huduma vizuri
Epuka upendeleo katika utoaji wa huduma
Epuka rushwa
Wafanyakazi hawatatumia vifaa vya umma kwa faida binafsi wala kutafuta au kukubali neema au ushawishi.
Kuwa wa kweli, waaminifu, wa haki na thabiti katika shughuli zote
Kukubali utu wa mtu
Kuzingatia mahitaji ya watu na kuunga mkono kwanamna zinazolinda heshima zao.
Halmashauri ya Wilaya inajiweka yenyewe katika njia ya ushirikishwaji, inayohusisha wadau wa ndani na nje katika mchakato wa kufanya maamuzi.
Halmashauri ya Wilaya inafanya kazi kama timu ya pamoja ili kuongeza umakini na ufanisi
Halmashauri ya Wilaya na wafanyakazi wa mashirika wanapaswa kuweka kando kipaumbele na mapendekezo yao binafsi ili kutumikia matakwa ya Taasisi na yale ya wateja wao.