• Malalamiko |
    • Anuani Zetu |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Kilwa District Council
Kilwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Mikakati ya Halmashauri
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Utumishi na Utawala
      • Elimu ya Msingi
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Maliasili
    • Vitengo
      • Usafi na Mazingira
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Biashara
      • TASAF
      • Lishe
      • Uvuvi
    • Miji Midogo
      • Masoko
      • Kivinje
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za Uwekezaji
    • Biashara na Viwanda
    • Madini
    • Uvuvi
    • Utalii
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Mikopo kina Mama na Vijana
    • Huduma za Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayo tekelezwa
  • Machapisho
    • Muongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Mifumo
    • PlanRep
    • FFARS
    • Prem
    • Salary Slip Portal

Fedha na mipango


Kamati hii inawashirikisha wenyeviti wa Kamati zote za Kudumu na inapaswa kukutana kila mwezi mara moja. Aidha, madaraka ya Kamati hii ni kama ya Kamati zingine za Kudumu na hivyo hairuhusiwi kisheria kufanya kazi/majukumu ya Kamati zingine za Kudumu. Kwa ujumla, majukumu yake ni pamoja na kusimamia na kudhibiti ukusanyaji wa mapato na matumizi ya mali ya Halmashauri kwa kupitia vikao vyake.

Majukumu Maalum ya Kamati:

  1. Kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wa mapato
  2. kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti na mpango wa Maendeleo kwenye Halmashauri ili kuidhinishwa na Halmashauri.
  3. kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mali za Halmashauri, ukusanyaji wa mapato, kufuta madeni, na kuomba vibali Maalum kwa matumizi yanayohitaji kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
  4. kufikiria na, pale inapowezekana, kupendekeza kwenye Halmashauri masuala yanayohusu Sheria Ndogo na utendaji katika ngazi za chini za Halmashauri.
  5. kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili matumizi ya mafungu ya fedha (re-allocation) yaliyopo katika makisio yaliyoidhinishwa na kuyapeleka kwa Halmashauri.
  6. kuratibu mapendekezo kutoka kwenye Kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyawasilisha kwenye Halmashauri.
  7. kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashauri mikopo yote ya Halmashauri.
  8. kutoa mapendekezo ya vitega uchumi kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290.
  9. kupokea na kujadili taarifa za wakaguzi wa fedha na mali ya Halmashauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na maelekezo na maoni ya wakaguzi kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa, Sura ya 290.
  10. Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za Halmashauri, kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Waziri na taratibu nyingine zitakazowekwa na Halmashauri;
  11. Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwa hususan kuhusu taratibu za fedha, ikiwa ni pamoja na mapitio ya mara kwa mara yanayohusu thamani ya fedha ambapo Kanuni mbalimbali za manunuzi ya mali na vifaa hutumika;
  12. Kufikiria na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali, vinavyotolewa na Halmashauri;
  13. Kufikiria mapendekezo ya Bajeti na Mipango ya Maendeleo ya kila Kamati ya Kudumu na kuiwasilisha kwenye Halmashauri ili kupata idhini;
  14. Kushughulikia tofauti ya mapato na matumizi katika bajeti yote na kupendekeza hatua stahiki ya kuchukua kuondoa mapungufu katika mapato au ziada matumizi;
  15. Kufikiria mapendekezo yote yanayohusu matumizi makubwa ya fedha kabla hayajawasilishwa kwenye Halmashauri ili kupata idhini;
  16. Kupokea mahesabu ya mwaka ya Halmashauri na kuhakikisha taarifa ya mahesabu ya mwaka inawasilishwa kwa wakati kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
  17. Kupitia na kuidhinisha mpango wa manunuzi wa Halmashauri kwa kuzingatia mpango wa Bajeti uliopitishwa na Halmashauri;
  18. Kupitia taarifa ya kila robo mwaka kuhusu Manunuzi iliyowasilishwa na Afisa Masuuli;
  19. Kusimamia utekelezaji wa mikataba ya Halmashauri kwa kukagua miradi inayotekelezwa na vifaa vilivyopokelewa;
  20. Kumwelekeza Mkurugenzi kufanya manunuzi au ukaguzi wa huduma au vifaa vilivyonunuliwa ili kupata thamani halisi, itafanyika hivyo endapo itadhihirika kwamba, maelezo yaliyotolewa kuhusu manunuzi ya vifaa au huduma hayaridhishi;
  21. Kuidhinisha majina ya wajumbe wa Bodi ya zabuni na wa Bodi zingine kwa mujibu wa Sheria husika;
  22. Kushughulikia orodha ya wadaiwa wote itakayokayowasilishwa kwenye Kamati na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua;
  23. Kupendekeza njia na taratibu za kuondosha vifaa chakavu. Uondoshaji wa vifaa unaweza kufanyika kwa njia ya kuuza au kuviharibu;
  24. Kujadili na kupitia taarifa za fedha za kila mwezi na kila robo mwaka;
  25. Kupendekeza kwa Halmashauri hatua za kuchukua kuhusu kufuta madeni ya Halmashauri;
  26. Kushughulikia Sera kuhusu kukopa na uwekezaji,
  27. Kujadili na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali vinavyotozwa na Halmashauri, 
  28. Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano na Halmashauri nyingine.
  29. Kurekebisha na kusimamia makusanyo na matumizi ya mapato ya vijiji na miji midogo kwa mujibu wa Sheria, Sura ya 287.
  30. kuteua wakaguzi wa fedha/mali za Serikali za Vijiji kwa mujibu wa Sheria, Sura ya 290.
  31. Kujadili na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kuhusu mambo yote ya yanayohusu masuala ya ajira na kinidhamu ya wafanyakazi na watumishi.
  32. Kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu nyumba za Halmashauri.
  33. Kupokea na kutoa uamuzi juu ya mapendekezo ya watumishi wanaokwenda masomoni.
  34. Kujadili na kupendekeza masuala yote yanayohusu maslahi ya jumla ya watumishi, ikiwa ni pamoja na mikopo, nyumba, usafiri, matibabu, rambirambi na motisha nyinginezo.
  35. Kupitisha mapendekezo ya kuthibitisha watumishi kazini baada ya kumaliza kipindi cha majaribio kulingana na miundo husika ya utumishi.
  36. kupendekeza Sheria Ndogo zinazohusu Kamati.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 04, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 11, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. April 25, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • BANDARI YA UVUVI KILWA KUKAMILIKA MWEZI JUNI 2025

    May 08, 2025
  • KAMATI YA SIASA YA CCM MKOA WA LINDI YAIPONGEZA KILWA KWA UTEKELEZAJI WA ILANI

    May 07, 2025
  • KILWA YAPIGA HATUA KATIKA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

    May 06, 2025
  • WANANCHI, WANAFUNZI NA WATUMISHI KILWA WAJITOKEZA KWA MAZOEZI YA PAMOJA UWANJA WA MWENGE/TAIFA

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Akipokea Mwenge wa Uhuru.
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • TARURA GPN
  • Watumishi Portal
  • MIKOPO 10%
  • Mikopo ya Wanawake na Vijana
  • Huduma za Elimu

Tovuti Muhimu

  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu
  • Lindi

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani Zetu

    Kilwa Masoko

    Anuani ya Posta: 160

    Simu: 0672365354

    Simu: 0672581557

    Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Kanuni Binafsi
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa