• Malalamiko |
    • Anuani Zetu |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Kilwa District Council
Kilwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Mikakati ya Halmashauri
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Utumishi na Utawala
      • Elimu ya Msingi
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Maliasili
    • Vitengo
      • Usafi na Mazingira
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Biashara
      • TASAF
      • Lishe
      • Uvuvi
    • Miji Midogo
      • Masoko
      • Kivinje
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za Uwekezaji
    • Biashara na Viwanda
    • Madini
    • Uvuvi
    • Utalii
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Mikopo kina Mama na Vijana
    • Huduma za Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayo tekelezwa
  • Machapisho
    • Muongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Mifumo
    • PlanRep
    • FFARS
    • Prem
    • Salary Slip Portal

maendeleo ya jamii

MAENDELEO YA JAMII                                                                                                                               

Idara ya Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana ni miongoni mwa Idara 10 na vitengo 4 vinavyojitegemea katika  Halmashauri ya Wilaya y Kilwa, na ni kiungo muhimu kati ya Halmashauri na jamii kwa kuratibu na kusimamia shughuli za Halmashauri. 

MUUNDO WA IDARA

Idara ina vitengo Vikuu Vitatu ambavyo ni:

  • Maendeleo ya Jamii kikiwa na watumishi 18
  • Ustawi wa Jamii kikiwa na watumishi 2  
  • Maendeleo ya Vijana kikiwa na Mtumishi1

 SHUGHULI  ZA IDARA. 

Maendeleo ya Jamii

  • Kushirikisha jamii katika kubaini, kubuni, kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi mbalimbali ya Maendeleo.
  • Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango/miradi ya Maendeleo.
  • Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana na watumishi wa sekta nyingine.
  • Kuelimisha viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali na viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu Sera mbali mbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
  • Kuelimisha na kuhamasisha jamii kupambana na VVU na UKIMWI.
  • Kueneza elimu ya Uraia mwema.
  • Kufanya uchambuzi wa matatizo ya jamii na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi zingine.
  • Kuvisaidia vikundi maalum (vya ushirika, vikundi vya kijamii, vya kidini, n.k.) kuandaa miradi na kuwaelekeza namna ya kupata mitaji.
  • Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia na kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia jinsia.
  • Kuhamasisha jamii kuondokana na mila/desturi zilizopitwa na wakati na kuwa na mtazamo wa kupenda kuleta mabadiliko.
  • Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya wanawake.
  • Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi na.
  • Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya watoto.
  • Kuratibu maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

 Ustawi wa Jamii

  • Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Miongozo, Kanuni na viwango vya ubora katika utoaji wa huduma mbalimbali za ustawi wa jamii.
  • Kufanya tathmini, ufuatiliaji na utaratibu wa huduma za ustawi wa jamii.
  • Kujenga uwezo wa kitaaluma kwa Maafisa Ustawi wa jamii ili waweze kutoa huduma timilifu kwa wananchi.
  • Kufanya tafiti zinazohusu huduma za ustawi wa jamii.
  • Kuwajengea uwezo watumishi wa ustawi wa jamii na Wadau katika utoaji wa huduma.
  • Kuanzisha na kuendeleza programu za kushawishi, kutetea na kulinda haki za makundi maalumu yakiwemo watu wenye ulemavu wa viungo na ngozi, wazee na wasiojiweza, familia zenye dhiki na watoto waishio katika mazingira hatarishi.
  • Kujenga Uhusiano na wadau wa nje na ndani ili kutoa huduma bora za ustawi wa jamii.
  • Kuratibu shughuli za mabaraza ya vijana.

Maendeleo ya Vijana

  • Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana.
  • Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya vijana.
  • Kuhamasisha vijana kufufua moyo wa kujitolea kwa ajili ya Maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
  • Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha, stadi za kazi na Afya ya uzazi na kujamiina kwa Vijana.
  • Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, ajira kwa vijana na elimu ya familia kwa kushirikiana na Vyama visivyo vya kiserikali.
  • Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu vijana.
  • Kuratibu shughuli za NGOs mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya Vijana.
  • Kuandaa mpango wa kuboresha malezi ya vijana.
  • Kuhamasisha waajiri na wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo nafuu kwa vijana katika maeneo mbalimbali.
  • Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo vijana ili kuwawezesha kujiajiri.
  • Kuandaa mipango ya kuhamasisha vijana ili kuanzisha miradi midogo midogo ya kujiajiri.
  • Kuratibu shughuli za mabaraza ya vijana.
  • Kuandaa na kuratibu shughuli za matamasha ya vijana.
  • Kuratibu shughuli za usajili wa NGOs na CBOs zinazofanywa ngazi ya Wilaya.
  • Kuratibu mafunzo ya  utoaji wa mbinu za kuwasaidia vijana kujikomboa na umaskini, ujinga, kupiga vita UKIMWI, madawa ya kulevya na kutetea usawa wa jinsia


Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 04, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 11, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. April 25, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • BANDARI YA UVUVI KILWA KUKAMILIKA MWEZI JUNI 2025

    May 08, 2025
  • KAMATI YA SIASA YA CCM MKOA WA LINDI YAIPONGEZA KILWA KWA UTEKELEZAJI WA ILANI

    May 07, 2025
  • KILWA YAPIGA HATUA KATIKA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

    May 06, 2025
  • WANANCHI, WANAFUNZI NA WATUMISHI KILWA WAJITOKEZA KWA MAZOEZI YA PAMOJA UWANJA WA MWENGE/TAIFA

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Akipokea Mwenge wa Uhuru.
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • TARURA GPN
  • Watumishi Portal
  • MIKOPO 10%
  • Mikopo ya Wanawake na Vijana
  • Huduma za Elimu

Tovuti Muhimu

  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu
  • Lindi

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani Zetu

    Kilwa Masoko

    Anuani ya Posta: 160

    Simu: 0672365354

    Simu: 0672581557

    Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Kanuni Binafsi
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa