Francis G.Kafuku
Huduma mbalimbali zinazotolewa na zinazopatikana idara ya Fedha na Biashara ni;
Wananchi wa Wilaya ya KILWA kwa zaidi ya asilimia (60%) ni watu waliojiajiri kwenye sekta isiyorasmi.
Shughuli kubwa wanazofanya ni pamoja na usindikaji mdogo wa vyakula, utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama vile sabuni za kufulia, dawa za maji za kuoshea vyombo na sakafu, usukaji, uuzaji wa mazao ya kilimo uvuvi na ufugaji hasa kwenye masoko na magulio. Wapo baadhi ya wananchi ambao wameweza kurasimisha biashara zao na hivyo kuweza kuanzia viwanda vidogovidogo na vya kati na wachache viwanda vikubwa. Wilaya ya KILWA inayo zaidi ya viwanda vidogovidogo 1550 ambavyo vingi ni vya Useremala, usagaji wa nafaka, utengenezaji wa vyakula vya kuku, kuoka mikate, kutengeneza nguo hasa batiki n.k.
Changamoto kubwa iliyopo kwa sekta isiyo rasmi pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wamesharasimisha shughuli zao ni ubora wa bidhaa wanazotengeneza, ufungaji wa bidhaa, masoko, mtaji wa kuendeleza biashara zao, elimu ya biashara na usafiri.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa