HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA
|
|
|
|
IDARA YA UTAWALA NA RASILIMALI WATU
Idara ya Utawala na Rasilimali watu ina jumla ya watumishi 180 wakiwemo Mkurugenzi Mtendaji 1, Maafisa Utumishi 4, Watunza Kumbukumbu 8, Makatibu Muhsusi 8, Wahudumu wa Ofisi 9, Madereva/fundi 16 Watendaji wa Vijiji 85 na Watendaji wa Kata 13, walinzi 7, na watumishi 19 wa mkataba, watumishi hawa wanafanya kazi za kuhudumia wananchi kwa ujumla, pamoja kuhudumia Idara zingine 13 na vitengo 6 vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya.
Malengo Makuu ya Idara ni kutoa huduma bora kwa kasi na viwango kwa kuzingatia usawa.
Kazi na Majukumu ya Idara
UTAWALA BORA.
Idara ya Utawala imekua ikihakikisha misingi ya utawala bora inaimarishwa kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata na Halmashauri kwa kuhimiza uwazi na uwajibikaji, ushirikishwaji wa wananchi na kutoa elimu ya kukataa kutoa rushwa na kuhakikisha vikao vyote vya kisheria vinafanyika katika ngazi zote ambazo ni vikao vya Serikali za vijiji, mikutano Mikuu ya Vijiji, Kamati za Maendeleo za Kata na vikao vya Halmashauri na Baraza la Madiwani.
IDADI YA WATUMISHI
Hadi kufikia tarehe 31 Disemba , 2016 Halmashauri ina jumla ya watumishi 1899 katika mchanganuo ufuatao kwa kila Idara: -
NA. |
IDARA |
IDADI YA WATUMISHI |
|
UTAWALA, FEDHA, UGAVI NA MAENDELEO YA JAMII
|
251
|
|
ELIMU MSINGI
|
870
|
|
ELIMU SEKONDARI
|
315
|
|
AFYA
|
366
|
|
UJENZI
|
10
|
|
MAJI
|
24
|
|
MIFUGO
|
15
|
|
KILIMO
|
48
|
|
Jumla
|
1899
|
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa