Taasisi ya Wajibu Institute of Public Accountability kwa kushirikiana na Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) kupitia programu ya kuwezesha makundi maalum katika mikakati ya ununuzi wa umma, imetoa mafunzo kwa wajasiriamali, Maafisa Manunuzi pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhusu matumizi ya mfumo wa manunuzi ya kielektroniki.
Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 1 Septemba 2025 katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa, ambapo makundi maalum hususan vikundi vya wajasiriamali vimeshauriwa kujiunga na mfumo wa NeST ili kuweza kunufaika na fursa mbalimbali za ununuzi wa umma.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Manunuzi wa PPRA Ndg. Tumpe Ngala ameeleza kuwa katika mfumo wa manunuzi ya umma, serikali imetenga asilimia 30 ya zabuni mahsusi kwa ajili ya makundi maalum ya kijamii na kijiasiliamali, ambazo zitawawezesha kupata na kushiriki fursa za tenda katika taasisi za kiserikali.
Nae mwezeshaji Ndg. Damas Makweba amesema mfumo wa manunuzi ya umma utawawezesha kupata taarifa za wazabuni kwa haraka na usawa kutokana na fursa ya uwezeshaji wa wajasiliamali wadogo na makundi maalum kuwez kushindana kwa usawa na kupata nafasi katika soko la umma hivyo amewataka wanavikundi kuhakikisha wanatumia kikamilifu mfumo wa NeST ili kupata Zaidi fursa zilizopo.
Aidha Afisa ufuatiliaji na tathimini kutoka Wajibu Institue Ndg. Tekra Mleleu amewataka wanavikundi waliopata mafuzo hayo kwenda kutoa elimu kwa jamii ili kuongeza uelewa na ushiriki mpana Zaidi katika fursa za ununuzi wa umma
Mafunzo haya yametolewa na Taasisi ya Wajibu Institute of Public Accountability kwa kushirikiana na Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) ikifadhiliwa na ubalozi wa Swedeni na ubalozi wa Falme za Norway.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa