Madini ni sekta nyingine ya kiuchumi ambayo ni muhimu katika ujenzi wa uchumi, lakini haijawa na tija sana kwa uchumi wa wilaya ya Kilwa kwasababu hakuna wawekezaji wa kutosha kuweza kuwekeza katika uchimbaji wa madini, uchimbaji uliopo katika maeneo machache ni wa kiwango kidogo kwa kuwa wanaojihusisha katika shughuli hii ni wachimbaji wadogo ambao hawana nyenzo za kuweza kuifanya sekta ya madini iwe na tija katika Wilaya ya Kilwa.
Wilaya ya kilwa ina Maeneo ambayo madini yamekuwa yakipatikana ambayo ni madini ya gasi Maeneo ya Makangaga, Mbwemkuru na Kiranjeranje, uwepo wa mafuta na gesi katika eneo la kijiji cha Kiswele na Rushungi mwambao mwa Bahari ya Hindi na baadhi ya Maeneo katika kijiji cha Songosongo.
Hivyo Wilaya ya Kilwa inawakaribisha wawekezaji kuja na kuwekeza katika hekta 300 za uchimbaji wa madini ili kuleta ushindani na ufanisi katika sekta ya madini na gesi ili kukuza uchumi wa Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa