Ndg.Israel Mhando
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa halmashauri zinazotekeleza miradi ya TASAF nchini. Imekuwa ikitekeleza miradi ya TASAF kuanzia TASAF I, TASAF II na sasa TASAF III ambayo inahusu mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN).
Katika mpango wa kunusuru kaya maskini Halmashauri imetambua na kuandikisha kaya zipatazo 5,922. Hadi sasa kaya zipatazo 5,699 ndizo zinazopata ruzuku baada ya kaya 213 kuondolewa kutokana na walengwa kufariki, kuhama na kaya 28 zilibainika kuwa ni za wajumbe wa Serikali ya Kijiji na kamati ya mradi ya TASAF (CMC). Zoezi la uwasirishwaji wa fedha linafanyika kila baada ya mwezi mmoja.
Pamoja na uwasirishwaji fedha, huduma nyingine inayotolewa ni ya ajira za muda.Katika kutekeleza huduma hii TASAF kupitia Halmashauri ya Wilaya imewezesha uendeshaji wa mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya Wilaya (PAA) pia imeibua miradi na kutoa mafunzo kwa kamati za mradi, wajumbe watatu wa serikali ya kijiji, mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kijiji.
Walengwa wa kaya maskini wanafanya kazi ambazo zina waongezea kipato, zinaendeleza miundombinu, zinawaongezea walengwa ujuzi na kuchangia mabadiliko ya tabia ya nchi, huduma hii ni ya hiari. Katika huduma hii 75% ya fedha za mradi ni ujira wa walengwa na 25% ni ununuzi wa vifaa.
Pia kuna huduma ambayo inatarajiwa kuanza ya kuweka akiba. Katika huduma hii walengwa wa kaya maskini wataungana katika vikundi vya watu wasiopungua kumi (10) na wasiozidi kumi na tano (15),Vikundi hivi vita weka akiba kutokana na vyanzo vya mapato mbalimbali ambavyo wata vibaini baada ya kupewa mafunzo (maelekezo).
Hudumaya ujenzi wa miundo mbinu nayo itafanyika katika vijiji vyote 58 ambavyo vina walengwa wa mpango. Miundo mbinu hiyo itajikita kwenye sekta ya Afya, Elimu na Maji.
Pamoja na majukumu mengine,hayo ni baadhi ya majukumundani ya TASAF III.
PAMOJA TUONDOE UMASKINI
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa