Benki ya CRDB wilayani Kilwa imekabidhi msaada wa meza 40 na viti 40 vyenye thamani ya shilingi 3,200,000/= kwa Shule ya Sekondari Mavuji iliyoko Wilayani Kilwa, ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha mazingira ya elimu wilayani Kilwa.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, 20 Septemba, 2025 Ndg. Ambele David Mwasabila, Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kilwa amesema, Msaada huo ni sehemu ya sera ya Uwajibikaji wa Kijamii (CSR) wa Benki ya CRDB, inayolenga kurudisha sehemu ya faida kwa jamii hususan katika sekta za elimu, afya na maendeleo ya kijamii.
Naye Bi. Jenifer Urassa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, ameishukuru Benki ya CRDB kwa mchango huo muhimu, huku akibainisha kuwa meza na viti hivyo vitasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kuinua ubora wa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mavuji.
Kwa upande wao wanafunzi na walimu wa shule hiyo wamefurahia msaada huo na kutoa shukrani zao za dhati kwa Benki ya CRDB, Aidha wameeleza kuwa meza na viti hivyo vitawawezesha kujifunza na kufundisha katika mazingira bora zaidi, jambo litakaloongeza ari ya ufaulu na kuinua kiwango cha elimu shuleni hapo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa