Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kupitia Idara ya Mipango na Uratibu imeendesha mafunzo maalum kwa Maafisa Bajeti wa kila idara na vitengo kwa lengo la kuongeza ufanisi katika maandalizi ya bajeti ya Halmashauri.
Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 19 Septemba 2025 katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa - Masoko.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mwezeshaji kutoka idara ya Mipango na Uratibu Ndg. Ayubu Matata amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa halmashauri wa kuimarisha matumizi sahihi ya rasilimali fedha.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kupanga bajeti zenye uhalisia ili kuendana na mahitaji halisi ya wananchi na mwelekeo wa serikali katika kuleta maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa inaendelea kujipanga kuhakikisha kila idara inakuwa na bajeti iliyoandaliwa kwa usahihi ili kufanikisha miradi ya maendeleo na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa