Kilimo ni uti wa mgongo Katika wilaya ya Kilwa ambapo zaid ya 80% ya wananchi wanajihusisha na shughuli mbalimbali za Kilimo ambapo takribani hekta 47,223 zinatumika kwa kilimo cha mazao ya chakula na mazao ya biashara. Mazao yanayolimwa kwa wingi katika wilaya ya Kilwa ni kama yafuatayo; kilimo cha muhogo, kilimo cha mtama, mbaazi, ufuta, viazi vitamu, kilimo cha machungwa, maembe, Nazi, kilimo cha Mwani, mbogamboga na mahindi.
Licha ya kuwa na maeneo mazuri ya kufanya shuguli za kilimo maeneo mengi ambayo yanarutuba hayatumiki ipasavyo kuweza kuleta tija katika sekta ya kilimo. Hali hii inatokana na wakulima wengi wamekuwa wakitumia nyenzoo duni za kilimo, ukosefu wa soko la uhakika wa mazao umepelekea wakulima kutokuwa na ari ya kufanya kilimo kama sekta muhimu ya kuwakwamua katika wimbi la umaskini, upungufu wa wataalamu katika sekta ya kilimo, ukosefu wa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, ukosefu wa mitaji kwa wakulima na ukame.
Kwa kupitia changamoto zinazoikabiri sekta ya Kilimo Wilaya inawakaribisha wawekezaji kuja na kuwekeza katika maeneo yafuatayo katika sekta ya kilimo ili kuleta tija katika sekta ya Kilimo kwakuwa mazingira yaliyopo yanaruhusu:
A. Kuwekeza katika kilimo cha mbogamboga, matunda, matikiti, viazi vitamu, maembe, machungwa.
B. Viwanda vya kuchakata mafuta ya alizeti, nazi na ufuta
C. Viwanda vya kutengeneza bidhaa za mazao ya kilimo kama bidhaa zinazotokana na zao la muhogo, viazi vitamu, mahindi, matunda ya maembe na machungwa, mbaazi.
D. Kiwanda cha kutengeneza bia kutokana na zao la Mtama
E. Kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji ambapo kuna hekta zipatazo 10,322 ambazo hazijaanza kutumika kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji katika maeneo ya Mavuji, Makangaga, Matandu.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa