Ndg.M.R.Mumini (DSEO)
HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA
TAARIFA YA IDARA ZA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI KILWA FEBRUARI 2017
UTANGULIZI
Idara za Elimu Mingi na Sekondari zinajishughulisha na majukumu ya Kusimamia, Kuinua na Kuboresha Maendeleo ya Elimu Wilayani. Aidha huduma zinazotolewa ni: Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Ufundi Stadi, Elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu, Elimu ya sekondari, Elimu ya Watu Wazimu ambayo imagawanyika katika sehemu kuu nne nazo ni Elimu Nje ya Mfumo, Elimu ya Ufundi, Mukeja na MEMKWA.
Wilaya ina jumla ya shule za Msingi zilizosajiliwa 108 na shule za vitongoji (Satelite) 5 zenye jumla ya wanafunzi 52,127 kati yao wavulana ni 25,976 na wasichana 26,151.
UONGOZI
Idara ya elimu ina wakuu wawili. Ambao ni afisa elimu sekondari ndugu Mwinjuma Rajabu Mumini na afisa elimu msingi Ndugu Amosi Kabula. Viongozi wengine katika idara hizo ni afisa taaluma sekondari ndugu Ernestina Mduma, Afisa takwimu sekondari ndugu Khajui Bofu. Viongozi wengine wa idara ya elimu msingi ni Mafisa taaluma ndugu Musa Shabani na Yahaya Mdidima, maafisa takwimu na vielelezo ni Rehema Mkalola na Mshamu Ndandavale, Afisa elimu ya watu wazima ni ndugu Salumu Nampoto. Afisa elimu maalumu ndugu Mwanahiba Mwichande, Afisa Elimu kilimo ndugu Omari Mtimali, afisa utamaduni ndugu Emanuel Paul, afisa elimu sayansi kimu ndugu Rostabella Lilali, Afisa Elimu ufundi ndugu mshamu mkundi,
Afisa vielelezo ndugu mshamu kiwanda na ndugu Nafu apotei ambaye ni katibu mhutasi
Kwa upande wa Sekondari Wilaya ya Kilwa ina jumla ya Shule za Sekondari 27. Kati ya hizo shule 26 ni za Serikali na 01 inamilikiwa na taasisi ya Dini ya Kiislamu, shule za Sekondari zina jumla ya wanafunzi 5,906 ikiwa wavulana 2,763 na wasichana 3,143. Shule za serikali zina jumla ya wanafunzi 5,696 na Binafsi 210.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Idara ya Elimu Msingi ina mahitaji ya walimu 1,295 waliopo ni 787 na upungufu ni 508.
Idara ya Elimu Sekondari ina mahitaji ya walimu 408, walimu waliopo ni 294 na ina upungufu wa walimu 114 kati yao 98 ni walimu wa masomo ya sayansi na Hisabati.
3.0IDARA YA ELIMU MSINGI
2.1 UANDIKISHAJI
Wilaya inaendelea Kuandikisha wanafunzi wa darasa la Awali na Darasa la Kwanza kama ifuatavyo:-
AWALI |
DARASA LA KWANZA |
||||||||||||
MAOTEO
|
UTEKELEZAJI
|
MAOTEO
|
UTEKELEZAJI
|
||||||||||
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
% |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
% |
4,220 |
4,053 |
8,273 |
2,056 |
2,162 |
4,218 |
50.98 |
3,441 |
3,146 |
6,587 |
4,071 |
4,008 |
8,079 |
122.65 |
2,2 MIUNDOMBINU (Madarasa, nyumba na vyoo)
Aina ya Majengo
|
Mahitaji |
Yaliyopo
|
Upungufu
|
Vyumba vya madarasa
|
1150 |
732 |
418 |
Nyumba za walimu
|
787 |
303 |
484 |
Matundu ya vyoo
|
2354 |
673 |
1618 |
2.3 MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA DARASA LA NNE (SFNA) MIAKA MIWILI (2015- 2016)
Shule za Msingi 106 zilisajili watahiniwa waliofanya upimaji wa Kitaifa wa darasa la IV 2015, na mwaka 2016 shule 103 zilisajili watahiniwa wa upimaji wa Kitaifa, taarifa za wanafunzi walioanza darasa la kwanza, waliosajiliwa kufanya upimaji, waliofanya, wasiofanya, waliofaulu na waliofeli zimeoneshwa katika jedwali lifuatalo:-
MWAKA |
WALIOANZA DARASA LA I 2012 & 2013 |
WALIOSAJILIWA |
% |
WALIOFANYA MTIHANI |
% |
WASIOFANYA MTIHANI |
% |
WALIOFAULU MTIHANI |
% |
WALIOFELI |
% |
||||||||||||
WAV |
WAS |
JML |
WAV |
WAS |
JML |
|
WAV |
WAS |
JML |
|
WAV |
WAS |
JML |
|
WAV |
WAS |
JML |
|
WAV |
WAS |
JML |
|
|
2015 |
3298 |
3190 |
6458 |
2692 |
2775 |
5467 |
84.65 |
2306 |
2538 |
4844 |
88.6 |
385 |
237 |
622 |
11.4 |
1904 |
2047 |
3952 |
81.56 |
402 |
3190 |
6488 |
2692 |
2016 |
3413 |
3341 |
6754 |
2438 |
2561 |
4999 |
74 |
2261 |
2452 |
4713 |
94.2 |
177 |
109 |
286 |
5.7 |
1992 |
2170 |
4162 |
88.31 |
269 |
282 |
551 |
11.69 |
Hali ya ufaulu ni ya kuridhisha kwa kuwa ufauli umekuwa ukipanda mwaka hadi mwaka, mwaka 2015 ufaulu ulikuwa asilimia 81.56 na mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 88.31, ufaulu ulipanda kwa asilimia 6.75.
2.4: MATOKEO YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE) MIAKA MIWILI (2015- 2016)
Wilaya ya Kilwa ina jumla ya shule za Msingi 108, shule 104 zilifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2015 na shule 103 ndizo zilizokuwa na wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi kwa mwaka 2016, taarifa za wanafunzi walioanza darasa la kwanza, waliosajiliwa kufanya mtihani, waliofanya, wasiofanya, waliofaulu na waliofeli, zimeoneshwa katika majedwali yafuatayo:-
MWAKA |
WALIOANDIKISHWA DRS LA I |
WALIOSAJILIWA |
WALIODONDOKA |
WALIOFANYA |
WALIOFAULU |
WALIOFELI |
WASIOFANYA |
|
||||||||||||||||||
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
% |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
% |
WV |
WS |
JML |
% |
WV |
WS |
JML |
% |
|
|
|
||||||||||||||||||||||||||
2015 |
3363 |
3134 |
6497 |
1782 |
2050 |
3822 |
1581 |
1094 |
2675 |
41 |
1631 |
1937 |
3568 |
997 |
1027 |
2024 |
56.7 |
634 |
910 |
1544 |
43.3 |
151 |
103 |
254 |
6.6 |
|
2016 |
3152 |
2898 |
6050 |
1771 |
1955 |
3726 |
1381 |
943 |
2324 |
38.4 |
1741 |
1927 |
3668 |
1122 |
1133 |
2255 |
61.5 |
619 |
794 |
1413 |
38.5 |
30 |
28 |
58 |
1.56 |
|
Hali ya ufaulu ni ya kuridhisha kwa kuwa ufaulu umekuwa ukipanda mwaka hadi mwaka, mwaka 2015 ufaulu ulikuwa asilimia 56.7 na mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 61.5, ufaulu ulipanda kwa asilimia 4.8.
IDARA YA ELIMU SEKONDARI
3.1 UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2017
Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2017 ni 2334, wakiwemo wavulana 1111 na wasichana 1,223. Hadi kufikia tarehe 17/02/2017 jumla ya wanafunzi 2,089 wakiwemo wavulana 1008 na wasichana 1,081 wamesharipoti shuleni. Hii ni sawa na asilimia 90 ya wanafunzi wote waliotakiwa kujiunga na kidato cha Kwanza. Idadi ya wanafunzi ambao hawajaripoti mpaka sasa ni 245, wavulana 103 na wasichana 142 sawa na asilimia 10. Halmashauri bado inafanya ufuatiliaji wa wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni ili wote waweze kuripoti shuleni. Jedwali la kuonyesha uandikishaji limeambatanishwa katika taarifa hii.
Kuanzia tarehe 11/07/2016 Halmashauri ilitarajia kupokea wanafunzi wapatao 86 ambao ndio walipangwa. (Kilwa sekondari wavulana 46 na Ilulu sekondari wasichana 40) wa kidato cha tano. Wanafunzi wote hawa ni wa mchepuo wa HKL. Wanafunzi walioripoti ni kwa shule zte mbili walikuwa 61 na waliohama au kwenda shule binafsi ni 16, na waliohamia ni 2. Hadi kufikia tarehe 17/02/2017 wanafunzi waliopo ni 48, ambapo Shule ya Sekondari Kilwa wapo wanafunzi 24 na shule ya sekondari Ilulu wako wanafunzi 24.
3.3 MIUNDOMBINU NA SAMANI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
Lengo kwa sasa ni kuimarisha shule zilizopo kwa kuongeza Madarasa, Maabara, Hosteli na Nyumba za walimu. Ili kukabiliana na tatizo la mimba pamoja na utoro kwa wanafunzi Halmashauri imeweza kujenga hosteli 36 katika Shule za Sekondari 16. Pamoja na uwepo wa hosteli hizo bado kuna tatizo la wanafunzi kutokaa katika majengo hayo kutokana na tatizo la ukosefu wa samani za vitanda na ukosefu wa chakula. Aidha, kuna tatizo la upungufu mkubwa wa nyumba za walimu katika shule za sekondari, na upungufu wa maabara pamoja na matundu ya vyoo kwa ajili ya walimu na wanafunzi , kama inavyoonekana kwenye jedwali.
AINA YA MIUNDOMBINU |
MAHITAJI |
YALIYOPO |
UPUNGUFU |
Nyumba za walimu |
294 |
82 |
212 |
Vyumba vya madarasa |
198 |
185 |
13 |
Matundu ya vyoo vya wanafunzi |
256 |
229 |
27 |
Matundu ya vyoo vya walimu |
52 |
22 |
30 |
Maktaba |
26 |
3 |
23 |
Maabara |
78 |
19 |
59 |
Mabweni |
58 |
36 |
22 |
Mabwalo |
26 |
2 |
24 |
Jengo la utawala |
26 |
4 |
22 |
viti
|
5842 |
4682 |
1160 |
Meza
|
5842 |
4682 |
1160 |
NB. Upungufu wa madarasa upo kwenye baadhi ya shule hasa zenye wanafunzi wengi na baadhi ya shule zina ziada ya vyumba vya madarasa.
3.4 UJENZI WA MIUNDOMBINU YA SHULE
Wilaya inaendelea na ujenzi wa vyumba 13 vya Madarasa, utengenezaji wa viti na meza 1160 katika shule za sekondari Kilwa, Kivinje, Ali mchumo, Namayuni, Mpunyule, na Kiranjeranje kwa gharama ya shilingi 344,380,000 kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri. Ujenzi wa madarasa umefikia hatua ya umaliziaji. Utengenezaji wa viti na meza 1160 unaendelea ni mategemeo yetu kuwa ujenzi utakamilika mwishoni mwa mwezi machi 2017
3.4 UTOAJI WA CHAKULA
Katika Wilaya ya Kilwa shule zinazotoa chakula kwa wanafunzi ni shule ya sekondari ya wasichana Ilulu na shule ya sekondari ya Kilwa kwa wanafunzi wa kidato cha tano.
3.5 MATOKEO YA UPIMAJI WA KIDATO CHA PILI KWA MIAKA MIWILI (2015 – 2016)
Matokeo ya upimaji wa mitihani ya kidato cha pili (FTNA) kwa kipindi cha miaka miwili (2015-2016) katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa yameonesha kuongezeka kwa asilimia 6.5 Wanafunzi waliofanya mitihani mwaka 2015 walikuwa 1153,waliofaulu walikuwa 955 sawa na asilimia 83 na waliofeli walikuwa 198 sawa na asilimia 17. Kwa mwaka 2016 wanafunzi waliofanya mitihani walikuwa 1200, waliofaulu ni 1074 sawa na asilimia 89.5,na waliofeli ni 126 sawa na asilimia 10.5
Jedwali la ufaulu mwaka 2015 na 2016.
Mwaka |
Jumla ya waliofanya |
Daraja |
Waliofeli |
% ya waliofaulu |
|||
|
|
I |
II |
III |
IV |
|
|
2015 |
1153 |
28 |
98 |
188 |
641 |
198 |
83 |
2016 |
1200 |
68
|
128
|
205
|
673
|
126 |
89.5 |
Majedwali yafuatayo yanaonesha ufaulu kwa kila shule
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2015 na mwaka 2016 hayakuwa mazuri sana kama inavyoonekana kwenye jedwali la matokeo kwa miaka husika.
Mwaka
|
Jumla ya watahiniwa
|
Daraja |
Jumla ya Waliofaulu
|
% ya ufaulu
|
Waliofeli
|
% ya waliofeli
|
||||
I
|
II
|
III
|
IV
|
|
|
|
|
|||
2015
|
1110
|
2
|
32
|
88
|
460
|
582
|
52.17
|
528
|
47.83
|
|
2016
|
1043
|
1
|
46
|
116
|
426
|
589
|
56.0
|
454
|
43.2
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Hali ya ufaulu kwa kidato cha nne kwa miaka hiyo miwili inaonesha kuongezeka kwa asilimia 4 ijapokuwa bado asilimia ya ufaulu iko chini. Nafasi ya wilaya kitaifa kwa mwaka 2015 imekuwa ya 164 kati ya 178, na kwa mwaka 2016 Wilaya yetu imeshika nafasi ya 158 kati ya 178. Majedwali ya kuonesha ufaulu wa wanafunzi kwa miaka hiyo miwili yameambatanishwa.
4.0 MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA ELIMU
Ongezeko la uandikishaji wanafunzi wa kidato cha kwanza umeongezeka kutoka asilimia 72.1 mwaka 2016 na kuwa asilimia 90 kufikia mwezi wa Februari 2017.
Ongezeko la uandikishaji wanafunzi wa darasa la kwanza umeongezeka toka asilimia 109.3 kwa mwaka 2016 na kufikia asilimia 122.65 kwa mwezi Februari, 2017.
Ongezeko la ufaulu kwa matokeo ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne kutoka asilimia 81.56 mwaka 2015 hadi asilimia 88.31mwaka 2016, darasa la saba ufaulu ulipanda kutoka asilimia 56.7 mwaka 2015 hadi asilimia 61.5 mwaka 2016, kidato cha pili ufaulu wa upimaji uliongezeka kutoka asilimia 83 mwaka 2015 hadi asilimia 89.5 mwaka 2016 na kidato cha nne ufaulu uliongezeka kutoka asilimia 52.17 mwaka 2015 hadi 56 mwaka 2016.
Shule kutokaguliwa na kutembelewa mara kwa mara.
Naomba kuwasilisha.
…………………..
ZABLON, I. BUGINGO
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa