Wanawake wa kata ya Tingi Wilayani Kilwa kutoka Taasisi ya SAYDAT NAFISA TINGI FOUNDATION (SANATI) wameandaa Dua maalum kwaajili ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake ndani ya Miaka 4 na kuliombea Taifa kwa ujumla hususani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.
Hafla hiyo imefanyika Tarehe 08 Juni 2025 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ilulu ambapo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Dini wakiongozwa na Shekhe wa Wilaya ya Kilwa Shekh. Hussein Simo, Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Mohamed Nyundo.
Akizungumza Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amewapongeza wanawake hao kwa kuandaa Dua hiyo maalumu kwaajili Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani inaonyesha upendo mkubwa katika kumuunga mkono mhe. Rais katika uwajibikaji wake wa kulijenga Taifa.
Aidha Mhe.Telack amewapongeza Viongozi wa Dini kwa kuijenga jamii hiyo katika Misingi ya Dini na Imani, pia amewasihi kuendeleza desturi ya kuiombea Nchi na Viongozi wake kama walivyoanza katika hatua hiyo Nzuri.
Naye Shekh wa Wilaya ya Kilwa Shekh. Hussein Simo ameisisitiza jamii kuelekea Uchaguzi Mkuu kwenda kuchagua viongozi bora wenye maadili na uadilifu ili kuleta maendeleo katika jamii na kujenga jamii iliyobora.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo amemshukuru Mkuu Mkoa Mhe. Telack kwa kuungana nao katika Dua hiyo na kutoa nasaha ambazo zitaenda kuwajenga wanawake hao na jamii kwa ujumla.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa