Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Hemed Magaro, ameongoza ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata za Masoko na Likawage, tarehe 14 Agosti 2025, akiwa ameambatana na timu ya ufuatiliaji kutoka ofisi ya halmashauri ambapo ziara hiyo imelenga kukagua utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwa kutumia fedha za serikali na wadau wa maendeleo, pamoja na kujiridhisha kuhusu ubora, thamani ya fedha na maendeleo ya kazi katika maeneo husika.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji na timu yake wametembelea Ujenzi wa shule mpya ya msingi eneo la Mihina wenye thamani ya Shilingi (202) kupitia mapato ya ndani. Pia mradi wa ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, shilingi milioni (40.0) kupitia fedha za mfuko wa jimbo, Ukarabati wa madarasa manne katika Shule ya Msingi Mzizima shilingi (43.4) kutoka mfuko wa Elimu na mapato ya ndani.
Pia ujenzi wa Madarasa matatu na Vyoo 6 katika shule ta msingi Liwiti fedha milioni (83.2) program ya Boost, Ujenzi wa matundu mawili ya vyoo vya walimu na uwekaji wa mfumo wa umeme Shule ya Sekondari Likawage shilingi milioni (6.9) Mfuko wa Elimu na jimbo. Katika kituo Shikizi Nanjumba fedha shilingi (2.0) miradi hiyo inalenga kuboresha mazingira mazuri kwa walimu na wanafunzi.
Umaliziaji wa ujenzi wa Zahanati mpya ya Liwiti, kwa shilingi milioni (115) na Ukarabati wa Zahanati ya Nainokwe wenye thamani ya shilingi milioni (3.0) ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha huduma za afya ngazi ya jamii.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Ndg. Hemed Magaro amesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya wasimamizi wa miradi na watumishi wa sekta husika, akieleza kuwa ni kupitia mshikamano na uwajibikaji ndipo miradi ya maendeleo inaweza kufanikishwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotarajiwa.
Ziara hii ni sehemu ya utaratibu endelevu wa halmashauri wa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa