Timu ya mpira wa miguu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imeanza vyema michuano ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) kwa kuibuka na ushindi wa goli 1–0 dhidi ya Babati TC, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi.
Mchezo huo umechezwa katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Tanga Tech, tarehe 16 Agosti, 2025. Katika mchezo huo Mhandisi Masunga Maduhu Masunga kutoka Kilwa DC ameipatia timu yake goli pekee lililopeleka ushindi muhimu kwa Kilwa.
Ushindi huu unatoa hamasa kubwa kwa kikosi cha Kilwa kuendelea kufanya vizuri katika michezo inayofuata ya hatua ya makundi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa