Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Hemed S. Magaro, ameongoza kikao cha kuwasilisha taarifa kuhusu mafanikio ya ziara ya mafunzo ya Mtandao wa BMU yaliyofanyika mkoani Tanga tarehe 24 Juni 2025. Lengo la kikao hicho ni kushirikisha viongozi wa BMU, wataalamu wa sekta ya uvuvi, na wadau mbalimbali juu ya ujuzi, teknolojia, na mbinu bora walizojifunza katika ziara hiyo.
Kikao hicho kimefanyika Tarehe 15 Agosti 2025 katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi kikilenga kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kusimamia na kulinda rasilimali za bahari kwa kutumia mifumo ya usimamizi shirikishi ambayo italetakwa tija jamii ya Wilaya hiyo.
wakiwasilisha wajumbe wa Mtandao wa BMU wameeleza kuwa wamejifunza mbinu bora za ukusanyaji wa mapato ya baharini kupitia mifumo ya usimamizi shirikishi ndani ya BMU ambapo walijifunza namna ya kuboresha utaratibu wa kukusanya mapato kutokana na leseni za uvuvi, ada za shughuli za baharini, na tozo nyingine.
Utengenezaji wa matumbawe bandia kama njia endelevu ya kulinda mazalia ya samaki. Teknolojia hii, ambayo tayari imefanikiwa katika maeneo ya Tanga, husaidia kuzuia uharibifu wa matumbawe ya asili, kutoa makazi kwa viumbe vya baharini, na kuongeza idadi ya samaki katika maeneo ya uvuvi, pia uhifadhi endelevu wa mazingira ya bahari. Iliwemo kudhibiti uvuvi haramu, na kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za utunzaji wa mazingira.
Akizungumza katika kikao hicho, Ndg. Magaro amesisitiza kuwa mafunzo hayo yana mchango mkubwa kwa ustawi wa sekta ya uvuvi wilayani Kilwa. Ameongeza kuwa teknolojia ya matumbawe bandia imemvutia zaidi kutokana na manufaa yake katika kuimarisha uhifadhi wa mazingira ya bahari, kuongeza tija kwa wavuvi, na kukuza uchumi wa jamii za wavuvi.
Vilevile, amezishukuru Halmashauri za Wilaya za Pangani, Mkinga na Muheza kwa mapokezi mazuri, mshikamano, na maarifa waliowapatia, akisisitiza kuwa ziara kama hizi zinapaswa kuendelezwa ili kuimarisha mtandao.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa