Maonesho ya madini yanayoendelea katika viwanja vya Madini wilayani Ruangwa, yameanza kwa mafanikio makubwa, yakifungua milango ya fursa lukuki kwa wananchi na wawekezaji ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika uzinduzi rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainabu Telack, Juni 11, 2025 ameeleza kuwa mkoa wa Lindi una hazina kubwa ya madini, ambayo sasa yanatumika kama chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wake. Maonesho haya ni sehemu ya jitihada za mkoa kuhakikisha utajiri wa rasilimali unawanufaisha wananchi moja kwa moja.
“Tunalenga kuwakutanisha wachimbaji wa madini, wafanyabiashara na wawekezaji ili washirikiane katika kukuza sekta ya madini na kuongeza thamani ya uchumi wa wananchi wetu,” amesema Mhe. Telack.
Maonesho ya mwaka huu yamevutia washiriki wengi zaidi ikilinganishwa na mwaka jana, ambapo zaidi ya watu 6,000 walihudhuria, wakiwemo wageni kutoka mataifa 14. Mafanikio hayo yanatoa matumaini makubwa kwa maendeleo ya sekta hii muhimu.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, tunachukua fursa hii kuwakaribisha wadau wote kuendelea kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya madini yanayopatikana katika wilaya yetu ambayo ni Dhahabu (Gold), Shaba (Copper), Kinywe (Graphite), Jasi (Gypsum), Madini ya Ujenzi na Chumvi. Tafiti zinaendelea kufanyika ili kugundua aina nyingine za madini zinazopatikana katika wilaya yetu.
Kaulimbiu ya mwaka huu:
“Madini na uwekezaji fursa ya Kiuchumi Lindi, Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025”
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa