Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Selemani Jafo (Mb) amefanya ziara rasmi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Leo Tarehe 17/09/2024. Ziara hii ikiwa ni juhudi za serikali kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na kuleta matokeo yanayotarajiwa kwa wananchi.
Katika ziara hii Mhe. Jafo ametembelea mradi wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi wenye thamani ya Sh. Bilioni 266 za kitanzania ulioko kilwa Masoko. Mh. Jafo amekiri kuridhishwa na hali ya utekeleaji wa mradi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 70% za utekelezaji.
Mhe. Jafo ametoa pongezi za dhati kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Zainab Telack, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Mohamed Nyundo, Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi pamoja na timu ya wakandarasi kwa utekelezaji mzuri wa mradi huu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Zainab Telack ametoa pongezi za dhati kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza kwenye sekta ya uvuvi kwani itaongeza tija wa wananchi wa Kilwa na Lindi kwa ujumla.
Katika Kuhitimisha Mh. Jafo ametoa wito kwa wakandarasi wengine kuiga mfano wa wakandarasi wanaotekeleza mradi huu kwani wanazingatia muda wa utekelezaji wa mradi na hivyo kuleta mapinduzi ya ujenzi.
Kauli mbiu "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa