Kamati na Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wake Mhe. Farida Kikoleka Diwani wa Kata ya Miguruwe imeendelea na ziara yake ya siku mbili (2) ya kutembelea na kugagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri kwa Robo ya Kwanza ya Mwaka 2024/2025.
Wakiwa katika ziara hiyo kamati imeweza kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo ukarabati wa Hospitali ya Wilaya kinyonga, mradi wenye thamani ya Tsh. 900,000,000/= fedha kutoka Serikali Kuu, Mradi huu unahusisha ujenzi wa Jengo la Upasuaji, jengo la Radiologia (Jengo la Mionzi), jengo la Maabara, Jengo la Mama na Mtoto pamoja na Jengo la Kichomea taka.
Pia kamati imetembelea Mradi wa Ufunguzi wa barabara ya Shule ya Sekondari Namatungutungu, Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi, barabara ya Kuingia jengo la Halmashauri Lingaula pamoja na Stendi ya Mabasi Nangurukuru wenye thamani ya Tsh. 152,000,000/= ikiwa ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmshauri.
Naye Mhe. Kikoleka kwa Niaba ya kamati hiyo ametoa shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Kilwa. Pia ametoa wito kwa Wataalamu wa Afya ndani ya Hospitali hiyo kutoa huduma nzuri zinazoendana na hadhi na uzuri wa majengo hayo. Mwisho ametoa wito kwa wataalamu na wasimamizi wa miradi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kuendelea kuzingatia matumizi sahihi ya fedha za Seriakli na kuzingatia thamani ya fedha katika miradi inayoendelea kutekelezwa ili iweze kuleta tija kwa wananchi wa Wilaya ya Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa