Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Farida Kikoleka Diwani wa Kata ya Miguruwe,
Imefanya ziara siku tarehe 28/10/2024 ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa Robo ya Kwanza ya mwaka 2024/2025.
Katika ziara hiyo kamati imetembelea mradi wa ujenzi wa jengo la zahanati ya Kijiji cha Ujamaa katika kata ya Njinjo wenye thamani ya TSh. 52,000,000/= ambayo ni pesa kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri. Mradi huo upo katika hatua za awali (Msingi na ujazaji wa kifusi).
Pia kamati imetembelea mradi wa ukamilishaji wa jengo la zahanati ya Miguruwe wenye thamani ya TSh. 50,000,000/=
Ikiwa ni pesa kutoka Serikali Kuu.
Aidha Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa zahanati ya Miguruwe Ndg. Shija Athanas Mpuya (Mganga Mfawidhi) ameomba kuongezewa bajeti kwa ajili ya kukamilisha jengo hilo kwani kwa sasa liko katikati hatua za umaliziaji.
Kwa upande wao wajumbe wa Kamati hiyo waliahidi kuomba Baraza la Madiwani liridhie kuongeza fedha za umaliziaji wa Zahanati hiyo ya Miguruwe. Pia wamemuagiza Mhandisi wa Halmshauri kufanya mchakato wa upatikanaji wa maji katika eneo la Mradi.
Pamoja na kutoa pongezi kwa kamati zinazosimamia ujenzi wa zahanati hizo, Mhe. Kikoleka amesisitiza matumizi mazuri ya pesa za Serikali hususani kwa Zahanati ya Njinjo kwani jengo hilo bado liko katika hatua za awali.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa