Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Rashid Msaka imefanya ziara ya Mafunzo katika ya Soko la Madini Mkoa wa Lindi iliyoko Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi tarehe 16 Novemba 2024.
Lengo la ziara hiyo ni kupata elimu juu ya madini yanayopatikana katika Mkoa wa Lindi hususani Wilaya ya Kilwa, Utaratibu unaotumika katika Soko la Madini, Sheria na Kanuni zinazosimamia madini lakini pia kupata Elimu juu ya mapato ya Halmashauri yanayotokana na chanzo cha madini.
Akizungumza mbele ya Kamati hiyo Mtaalam kutoka katika Tume ya Madini Mhandisi Dickson Joram ameeleza kuwa katika Mkoa wa Lindi madini yanayopatikana ni Madini ya Vito, Madini ya Viwandani na Madini ya ujenzi. Madini hayo yanapatikana katika Wilaya Kilwa, Ruangwa na Nachingwea.
Aidha Mhandisi Jorum ameeleza faida za Madini kwa Serikali ambapo ametaja kuwa ni Mrabaha 6.3%, Ushuru wa Huduma 0.3%, kodi ya Zuio 0.2%, Uchangiaji miradi ya Maendeleo ya Jamii, Fursa za Ajira na kuchochea ukuaji wa mji katika maeneo husika.
Pia Mhandisi Joram amehadi kuendelea kutoa ushirikianao Kwa Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na kwamba ofisi yake iko tayari kutoa elimu kwa wananchi juu ya madini, fursa zilizopo katika sekta ya madini lakini pia kuwahimiza wananchi kujiepusha na vitendo vya utoroshaji wa madini.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa