Katika muendelezo wa ziara ya siku mbili ya Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Rashidi Msaka, walitembelea Mgodi wa uchimbaji madini ya Nikeli unaoendeshwa na Kampuni ya Enprizon Limited kutoka Nchini China ulipo katika Kijiji cha Nanjirinji ‘A’ kata ya Nanjirinji Wilayani humo.
Lengo la ziara hiyo ni kukagua na kuhakiki utekelezaji wa sheria na taratibu zinazoongoza shughuli za migodi, kujiridhisha na kiwango cha mapato yanayotokana na mgodi huo kwenda Serikalini, Halmashauri ya Wilaya na Serikali ya Kijiji, Pia Kufuatilia utekelezaji wa uchangiaji wa Maendeleo ya Jamii (CSR), kuimarisha mahusiano baina ya mgodi na Serikali na kutatua changamoto zilizopo.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati hiyo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Jimmy (Raia wa China) ameeleza kuwa kampuni ya Enprizon Limited ilisajiliwa mwaka 2020 na inamiliki leseni 4 za uchimbaji wa madini (PML 4). Kampuni ilianza kufanya uchimbaji wa majaribio mwaka 2023 kisha kuanza uzalishaji rasmi baada ya msimu wa mvua mwezi Agosti 2024. Kampuni inaweza kuzalisha angalau Tani 450 kwa mwezi Pia kampuni inatoa gawio kwa serikali kulingana na matakwa ya kisheria.
Kamati imetoa pongezi kwa uongozi wa mgodi huo kwa namna wanavyotekeleza shughuli za uchimbaji wa madini hayo na kuchangia mapato katika serikali, pia imetoa wito kwa kampuni hiyo kuendelea kufuata sheria na taratibu za uchimbaji wa madini na uhifadhi wa mazingira.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa