ZIARA YA KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO KATIKA MGODI WA LIKOFIA NANJIRINJI KILWA.
Posted on: November 16th, 2024
Ziara ya Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango katika Mgodi wa Likofia Nanjirinji Kilwa.
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rashidi Msaka wamefanya ziara ya kutembelea mgodi wa uchimbaji madini ya dhahabu uliopo katika kijiji cha Ninjirinji Wilayani Kilwa.
Ziara hiyo imefanyika kwa lengo la kukagua na kuhakiki utekelezaji wa sheria na taratibu zinazoongoza shughuli za migodi, kujiridhisha na kiwango cha mapato yanayotokana na mgodi huo kwa Serikali, Halamashauri ya Wilaya na Serikali ya kijiji, kufuatilia utekelezaji wa uchangiaji wa maendeleo ya jamii (CSR), kuimarisha mahusiano baina ya mgodi na Serikali na kutatutua changamoto zilizopo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi huo Ndg. Daniel Bahati Francis ameeleza kuwa kiwango cha uzalishaji katika Mgodi huo kwa sasa kimepungua kutokana na changamoto za kupungua kwa kiasi kinachopatikana katika mgodi huo, kuibuka kwa migodi mipya katika maeneo mengine,
Uwepo wa wachimbaji wa majaribio na kutofanyika kwa utafiti katika maeneo ya uchimbaji.