Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ikiongozwa na Makamu Mkwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rashidi Msaka (Diwani wa Kata ya Likawage), imefanya Ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo katika kata ya Masoko na Mandawa Tarehe 23/01/2025.
Katika ziara hiyo kamati imetembelea mradi wenye thamani ya TSh. 362,200,000/= fedha kutoka Serikali kuu, kupitia mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu Sekondari (SEQUIP) kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni mawili yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 80 kila moja, vyumba vinne (4) vya madarasa na vyoo matundu sita (6) katika Shule ya Sekondari Mtanga iliyopo katika Kata ya Masoko.
Pia kamati imetembelea mradi wa ujenzi wa nyumba moja ya walimu (Two in one) Katika Shule ya Sekondari Mavuji iliyo katika Kata ya Mandawa wenye thamani ya Tsh.95,000,000/= fedha kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa SEQUIP. Mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu sasa upo katika hatua ya msingi na unatazamiwa kakamilika ndani ya siku 67.
Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi katika maeneo yote mawili, aidha wajumbe wamesisitiza matumizi sahihi ya fedha na kuzingatia kukamalisha miradi kwa wakati ili itumike na kuleta matokeo chanya kwa jamii.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa