Katika kuhakikisha ustahimilivu wa jamii za Pwani dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF) limeendelea na ziara yake Wilayani Kilwa kwa kutembelea wakazi wa Kata ya Songosongo tarehe 28/02/2025. Ziara hii imelenga kufanya mazungumzo na wananchi wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazotekelezwa na WWF pamoja na washirika wake.
Lengo la mazungumzo hayo ni kutathmini mzunguko wa fedha walionao wananchi kupitia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na shughuli za uhifadhi wa mazingira. Shughuli hizo ni pamoja na uvuvi endelevu wa pweza, usindikaji wa mwani, na uendeshaji wa mtambo wa kuzalisha barafu unaotumiwa kuhifadhi samaki na mazao mengine ya bahari.
Matokeo ya mazungumzo haya yataliwezesha WWF kupitia mradi wa Ocean Risk and Resilience Action Alliance (ORRAA) kuandaa mikakati madhubuti ya kuwawezesha wananchi kufanya biashara kwa ufanisi zaidi, kuongeza faida, na kuimarisha ustawi wa jamii zao.
Hii ni sehemu ya jitihada za WWF za kuhakikisha kuwa wananchi wa Pwani wananufaika na rasilimali zao kwa njia endelevu. WWF itaendelea kushirikiana na wananchi wa Kilwa kuhakikisha wanapata suluhisho la kifedha na kiuchumi utakaoboresha maisha yao.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa