Katika kuhakikisha ustahimilivu wa jamii za Pwani dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), limetembelea wakazi wa Kata ya Somanga Wilayani Kilwa Tarehe 27/02/2025 ili kufanya mazungumzo na wananchi wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazotekelezwa na WWF pamoja na washirika wake.
Lengo la mazungumzo hayo ni kutambua mzunguko wa fedha walionao kupitia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika shughuli za uhifadhi wa mazingira katika maeneo ya pwani kama vile kuongeza thamani mazao ya mwani, mazao ya asali, mbinu endelevu za uvuvi na usindikaji wa samaki.
Matokeo ya mazungumzo hayo yataliwezesha Shirika la WWF kupitia mradi wa Ocean Risk and Resilience Action Alliance (ORRAA) kuandaa muundo wa kuwawezesha kufanya biashara kwa namna nzuri yenye faida zaidi ili kujenga suluhisho la kifedha kwa ajili ya ustawi jamii hiyo.
Mazungumzo hayo yamefanyika kwa makundi ya wanawake wanaojihusisha na VICOBA, kundi la wasindikaji wa Mwani, kundi la wasindikaji asali. WWF wataendelea kufanya mazungumzo kwa wananchi wa kata ya Songosongo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa