Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo ameongoza wananchi Wilayani Kilwa kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo tarehe 09 Desemba 2024.
Katika maadhimisho hayo Viongozi wa Kiserikali, viongozi wa madhehebu ya Dini, Wakuu wa Taasisi za Umma na Mashirika Binafsi wameshirikiana na wananchi kufanya usafi wa mazingira katika kituo cha Afya Tingi, kupanda miti na kisha kumalizia kwa kufanya Kongamano la uhuru katika Shule ya Sekondari Ilulu iliyoko kata ya Tingi wilayani humo.
Akizungumza baada ya kukamilisha zoezi la u.safi na upandaji wa Miti, Mhe. Nyundo amewasihi wananchi kujivunia hatua kubwa ya maendeleo katika taifa letu ukilinganisha na kipindi cha mkoloni, kuweka mbele maslahi ya Taifa kwa kuwa wazalendo, kuunga mkono juhudi zinazoendelea kufanywa na Viongozi ili kuleta maendeleo ya taifa letu.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni, Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara: "Uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa maendeleo yetu".
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa