Kufuatia Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024 kote nchini, Wenyeviti wapya wapatao 32 wa vitongoji vya Mamlaka za Miji Midogo ya Kivinje na Masoko Wilayani Kilwa, wameapishwa rasmi ili kuanza utekelezaji wa majukumu yao, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kilwa Masoko, Mhe. Sadick Moses Simon, leo tarehe 28/11/2024 katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (FDC) Kilwa Masoko.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed S. Magaro, amewapongeza wenyeviti hao kwa kuaminiwa na wananchi kuongoza katika vitongoji vyao. Pia amewasisitiza kutambua jukumu kubwa liliko mbele yao la kuwawakilisha wananchi wanaowaongoza, kutatua kero za wananchi na kusimamia shughuli za maendeleo katika Vitongoji vyao. Aidha Ndg. magaro ametoa wito kwa viongozi hao kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia sheria na kanuni za nchi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa