KIlwa,
Waziri wa maji na umwagiliaji Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali ipo mbioni kuanzisha Mradi mkubwa wa maji katika Mto Mavuji Wilayani Kilwa.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Lindi.
Profesa Mbarawa Amesema mradi wa Maji utakaoanzishwa utakuwa suruhusho la tatizo la upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kilwa Hasa katika kata ya Pande na Lihimalyao ambako kuna matatizo ya maji.
Amesema mchakato wa kuanzisha mradi huo umekwisha anza na upo katika hatua za mwishoni na muda si mrefu utatekelezwa.
“Mradi huu unaweza ukachukuwa muda mrefu kidogo kukamilika laikini tuna amini pindi utakapo kamilika utakuwa umesaidia kutatua tatizo la maji katika baadhi ya vijiji hapa Wilayani Kilwa Hasa katika kata ya pande na Lihimalyao ambapo vyanzo vingi vimekua vikitoa maji yenye Chumvi, kwahiyo tuendelee kusimamia hii miradi ambayo tunayo kwa umakini mkubwa ili wananchi waendelee kupata huduma ya maji yaliyo safi na salama” alisema Profesa Mbarawa
Aidha amemtaka Meneja wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kilwa Masoko Mhandisi Issa Banda kuhakikisha huduma ya maji inaimarika na wananchi wanafaidika na huduma hiyo pamoja na kuongeza mapato kutoka milioni ishirini na moja inayopatikana sasa hadi milioni arobaini na tano.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kilwa Masoko Mhandisi Issa Banda amesema Mamlaka ya maji Kilwa inakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Madeni sugu kwa baadhi ya Taasisi za serikali, ukosefu wa gari la mfumo wa Maji taka, uchakavu wa miundo mbinu pamoja na Kukosa umeme wa uhakika hali ambayo ipelekea kuongeza kwa saa kadhaa kupandisha maji katika Matenki kwa ajili ya kusambaza kwa Wananchi.
“Sanjari na mafanikio Mheshimiwa waziri tuna changamoto ya Madeni sugu kutoka katika taasisi mbalimbali za serikali, laikini pia kuna kiasi cha maji ambacho kinapotea kutoaka na uchakavu wa miundo mbinu ambayo tunaitumia.
Lakini tatizo linguine ni ukosefu wa umeme wa uhakika ambao tunaweza kutumia katika shughuli zetu za kila siku, siku nyingine umeme unakuwa mdogo kwa maana ya Low voltage kitu ambacho kinakuwa kinaturudisha nyuma, Mheshimiwa tunaomba utusaidie kupata jenereta lenye uwezo mkubwa ili liweze kutusaidia” alihitimisha Banda
Awali akisoma taarifa kwa Mheshimiwa Waziri Kaimu Mhandisi wa Maji Wilaya ya Kilwa Bw. Badi Mussa amemuomba Waziri kuongeza idadi ya watumishi katika idara hiyo kwani kwa sasa watumishi ambao wapo ni wachache.
Kaimu Mhandisi wa Maji Wilaya ya Kilwa Bw. Badi Mussa akisoma taarifa kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa alipoitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (Picha: Ally Ruambo).
Akiwa Wilayani Kilwa Profesa Mbarawa alitembelea miradi mbalimbali ikiwemo chanzo cha maji kilichopo katika kijiji cha Mpara.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa