Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, leo ametembelea Wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi kwa ajili ya kukagua maeneo yaliyoathirika na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya kusini.
Katika Ziara hiyo Mhe. Majaliwa ametembelea Maeneo ya Matandu na Somanga Mtama, sehemu za barabara kuu ya Dar es Salaam – Lindi ambazo ziliharibika vibaya kutokana na mvua hizo na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara kwa muda.
Waziri Mkuu aliambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax,Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Tellack,na Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, Mhe. Francis Ndulane.
Katika hotuba yake fupi kwa wananchi na vyombo vya habari, Mhe. Majaliwa alieleza kuwa Serikali iko tayari kuchukua hatua za haraka kurejesha miundombinu hiyo muhimu ili kuhakikisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa unaendelea bila matatizo.
“Tumekuja kuhakikisha kuwa Serikali inachukua hatua za haraka kukarabati maeneo yaliyoathirika na kuhakikisha huduma muhimu zinaendelea kupatikana” alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha, alitoa wito kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni kuchukua tahadhari dhidi ya mafuriko na kuzingatia ushauri wa wataalamu wa hali ya hewa na maafa
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa