• Malalamiko |
    • Anuani Zetu |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Kilwa District Council
Kilwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Mikakati ya Halmashauri
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Utumishi na Utawala
      • Elimu ya Msingi
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Maliasili
    • Vitengo
      • Usafi na Mazingira
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Biashara
      • TASAF
      • Lishe
      • Uvuvi
    • Miji Midogo
      • Masoko
      • Kivinje
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za Uwekezaji
    • Biashara na Viwanda
    • Madini
    • Uvuvi
    • Utalii
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Mikopo kina Mama na Vijana
    • Huduma za Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayo tekelezwa
  • Machapisho
    • Muongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Mifumo
    • PlanRep
    • FFARS
    • Prem
    • Salary Slip Portal

WAZIRI MKUU AZINDUA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KIGOMA

Posted on: July 20th, 2024

WAZIRI MKUU AZINDUA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KIGOMA 

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) akigusa kishikwambi kuzindua uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura leo tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma. 

 

Mhe. Majaliwa baada ya kuzindua zoezi hilo alipata fursa ya kushuhudia kuandikishwa kwa mpiga kura na kumkabidhi kadi yake. 

 

Awali wakati akihutubia wananchi waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika uwanja wa Kawawa uliopo Halmashuauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Mhe. Majaliwa amewataka raia wote wa Tazania wenye sifa wajitokeze kujiandikisha kuwa wapiga kura na kuhakikisha kuwa wasio raia wa Tanzania hawaandikishwi kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

 

“Nitoe rai kwa kila mpiga kura aliyeandikishwa mwenye uhitaji wa kuboresha taarifa iwe kwa kurekebisha taarifa au kuhama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda lingine asisite kufika katika kituo cha kuandikisha kwani Tume imeshajipanga ili kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa”

 

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa zoezi hilo lina lengo la kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanapata na kutumia haki yao ya kikatiba kama ilivyobainishwa kwenye Ibara ya 5 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

 

Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amelitaka Jeshi la Magereza kuweka miundombinu wezeshi ili kuiwezesha Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kutekeleza wajibu wake wa kuandikisha wafungwa wenye vifungo chini ya miezi sita na mahabusu kwa ufanisi.

 

“Hii fursa ambayo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya kuwawezesha magereza kupiga kura ya kuchagua viongozi wanaowataka, hii mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu kutoa fursa kwa wafungwa na mahabusu kupiga kura wakiwa magerezani” 

 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewahakikishia watanzania kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuhakikisha kuwa chaguzi zote  zitakuwa huru na Haki.

 

Mhe. Majaliwa  amesisitiza kuwa zoezi hilo ni kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi na kwamba wasio raia wa Tanzanai hawahusiki.

 

“..anayetakiwa kaundikishwa hapa ni raia wa Tanzania tu. Hapa ni lazima tuwe wazalendo. Tusiruhusu mtu yeyote kutoka nje kujandikisha kuwa mpiga kura,” amesema.

 

Mhe. Majaliwa pia amevitaka vyama vya siasa kutumia ruhusa ya kisheria ya kuweka mawakala kila kituo, kuhakikisha wanachagua mawakala ambao wanatoka kwenye maeneo vilipo vituo vya kuandikisha wapiga kura ili wawaze kuwatambua watu wanaojiandikisha na uraia wao.

 

“Mawakala wa vyama vya siasa mnaowajibu wa kuwatambua wanaojiandikisha, naomba nisisitize hapa, lazima muwe wazalendo namba moja, uzalendo wenu utasaidia kuwatambua watu ambao sio raia.”

 

Kwa Upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiandanga amesema kuwa uzinduzi wa uandikishaji na uboreshaji, mchakato huo umeshirikisha wadau mbalimbali wa uchaguzi ikiwa ni utekelezaji wa falsafa ya 4R za Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

“Tume imekutana na wadau wa makundi mbalimbali kama vile Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia,Viongozi wa Dini, Makundi Maalum kama vile Vijana, Wanawake na watu wenye Ulemavu . Lengo ni kuhakikisha kuwa mchakato huu unakuwa shirikishi kwa watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vya siasa au dini”

 

Naye, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Jacobs Mwambegele amesema kuwa Jumla ya vituo 40,126 vitatumika katika zoezi la uboreshaji wa Daftari ambapo kati ya hivyo, vituo 39,709 vipo Tanzania Bara na vituo 417 vipo Tanzania Zanzibar. 

 

“Idadi hii ya vituo ni ongezeko la vituo 2,312 zaidi ikilinganishwa na vituo 37,814 vilivyotumika kuandikisha Wapiga Kura kwa mwaka 2019/2020”.)

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 04, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 11, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. April 25, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAONESHO YA MADINI RUANGWA 2025 YAWAPA WANANCHI FURSA MPYA ZA UWEKEZAJI

    June 11, 2025
  • KILWA NA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MAONESHO YA MADINI MKOANI LINDI

    June 11, 2025
  • WANAWAKE KATA YA TINGI WAANDAA DUA MAALUM KUMUOMBEA MHE. RAIS SAMIA

    June 08, 2025
  • DC KILWA AITAKA JAMII KUDHIBITI UTUMIAJI WA PLASTIKI ILI KUYALINDA MAZINGIRA.

    June 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Akipokea Mwenge wa Uhuru.
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • TARURA GPN
  • Watumishi Portal
  • MIKOPO 10%
  • Mikopo ya Wanawake na Vijana
  • Huduma za Elimu

Tovuti Muhimu

  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu
  • Lindi

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani Zetu

    Kilwa Masoko

    Anuani ya Posta: 160

    Simu: 0672365354

    Simu: 0672581557

    Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Kanuni Binafsi
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa