Katika kilele cha Maadhimisho ya Nane Nane Kanda ya Kusini, Mgeni Rasmi Mhe. Dkt. Seleman Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara, leo tarehe 08 Agosti 2025, ametembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na kutoa pongezi kwa namna ambavyo Halmashauri ilijipanga kushiriki kikamilifu katika maonesho hayo muhimu kwa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Waziri Jafo ametembelea mabanda ya wajasiriamali waliowakilisha Kilwa katika maonesho hayo na kushuhudia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ndani ya Wilaya ya Kilwa, zikiwemo zile zinazotokana na mwani, bidhaa za sanaa, viungo na usindikaji wa mazao, ambapo ameonesha kufurahishwa na juhudi za uongezaji thamani wa mazao na kuwaasa wajasiriamali kuongeza ubunifu na ubora wa bidhaa ili kuweza kuvuka mipaka ya masoko ya ndani na kufikia masoko ya kitaifa na kimataifa.
Pia, Mhe. Jafo ametembelea maeneo ya maonesho ya mifugo, bwawa la samaki na vitalu vya mazao mbalimba na kujionea kwa macho juhudi za Halmashauri katika kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya kisasa na tafiti katika kuongeza uzalishaji na tija.
Akizungumza na wataalamu na washiriki wa maonesho hayo, Mhe. Jafo ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa maandalizi mazuri, ubunifu na ushiriki wa kiwango cha juu unaodhihirisha dhamira ya dhati ya kuendeleza kilimo, mifugo na uvuvi kama mihimili mikuu ya uchumi wa wananchi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa