Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kushrikiana na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) wametoa Mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa e- Office kwa wataalamu wa Uhifadhi Taarifa (Masijala) wa Halmashauri ya Wilayani Kilwa,lengo ikiwa ni kuwapatia Elimu juu matumizi ya Mfumo wa usambazaji na utunzaji wa Taarifa Kidigital ili kuwa na urahisi wa ufuatilia wa utekelezaji wa taarifa mbalimbali kwa taasisi na Wananchi kwa ujumla.
Mafunzo hayo yametolewa Leo Tarehe 17 /03/2024 Katika Ukumbi wa Chuo Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa ambapo Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Ndg.Happynes Mabagalo amewahasa Watumishi kuwa na usiri katika katika ushughulikiaji wa kazi za Kiserikali kwa kuepuka kupokea taarifa kwenye mifumo isiyo Rasmi.
Kwa upande wake Mwezeshaji Innocent Mrema amesema moja ya Malengo ya utoaji wa Mafunzo Hayo ni kuelekeza juu ya upangaji wa taarifa vizuri, uandishi na jinsi ya kuingiza taarifa za Watumishi katika Mfumo wa Kidigitali pia amesema matumizi ya Mfumo huu unaenda kutatua changamoto ya kupotea kwa Nyaraka na kupunguza utegemezi wa makaratasi katika uhifadhi za nyaraka.
Aidha Ndg. Mrema amesema Mfumo wa e-OFFICE unalenga kurahisisha utunzaji wa nyaraka, kuimarisha uwazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za kiserikali ikiwemo kutoa huduma za haraka kwa wananchi pale wanapoleta maombi mbalimbali,ambapo wahifadhi taarifa kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kilwa wameelekezwa namna ya kutumia na kusimamia nyaraka kwa haraka, usalama na kwa usahihi.
Mafunzo haya yatatatolewa kwa siku saba kwa Maafisa Masuuli, Watumishi wa Masijala, Maafisa Watekelezaji,Wasimamizi Mfumo na Shabaha ya Mafunzo hayo ni kwenda kuanza Rasmi matumizi ya Mfumo wa e- Office katika Ofisi za Halmashuari ya Wilaya ya Kilwa
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa