kilwa,
Halmashauri nchini zimeshauriwa kutumia mfumo wa utunzaji taarifa za rasilimali na utoaji mafuta kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.
Ushuri huo umetolewa na Mtaalamu wa mifumo kutoka kampuni ya Day one softcom technologies Bw. Nsajigwa Mwakimbwala alipokua akifunga warsha ya siku saba ya mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo wa utunzaji taarifa za rasilimali na utoaji mafuta kwa kutumia mfumo wa kielektroniki, iliyofanyika katika ukumbi wa idara ya fedha katika halmshauri ya wilaya ya kilwa.
Bw. Nsajigwa amesema iwapo halmashauri zitaanza kutumia mfumo huo utawasaidia katika shughuli zao za kila siku “Nishauri tu halmshauri zingine ambazo hazijaanza kutumia mfumo huu waanze kuutumia kwakua utawasaidia katika shughuli zao”.
Pia Bw. Nsajigwa amezitaja baadhi ya faida ambazo zinapatikana kutokana na mfumo huu ikiwemo mpangilio mzuri wa upatikanaji wa taarifa, kujua matumizi sahihi ya mafuta, kuzuia upotevu wa kumbukumbu pamoja na kusaidia katika uandaji taarifa za kiuhasibu kuhusu rasilimali.
Kwa upande wao watumishi wameshukuru kwa mafunzo ambayo yamekua na tija katika kutimiza wajibu wao wa kila siku na kuahidi kuanza kutumia mfumo huo mara moja baada ya kukamilika kwa zoezi la uingizwaji wa taarifa katika mfumo huo.
Mafunzo hayo yalihudhuriwa na watumishi mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya kilwa wakiwemo wakuu wa idara na vitengo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa