watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wamepata Elimu ya Afya ya akili kutoka kwa Dkt. Pascal D. King'ria (Clinical Psychiatry ) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Meru, katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea Jijini Dodoma tarehe 19 Juni, 2025.
katika semina hii Dkt. Pascal amewahimiza watumishi kujenga uwezo wa kutambua hali na mapungufu yao lakini pia kutambua hali na mapungufu ya wengine katika mazingira ya kila siku na hususani mazingira ya kazi na nyumbani.
Aidha Ameelezea kuwa, katika kutimiza majukumu ya utumishi wa umma ni vema kuepuka mazingira ambayo yanaweza kuleta msongo wa mawazo na kusababisha afya ya akili ambayo yatahatarisha utendaji wa kazi na uwezo binafsi wa watumishi.
"Utulivu wa akili unachangia sana katika kuleta mafanikio katika mazingira ya kazi na jamii kwa ujumla" amesema Dkt. Pascal
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa