Kilwa,
Watumishi wametakiwa kufuata utaratibu wa kuacha kazi pindi wanapopata kazi sehemu nyingine.
Wito huo umetolewa leo na Katibu wa afya wilaya ya Kilwa ndugu John Maongezi katika mafunzo elekezi kwa watumishi wapya kada ya afya wilayani kilwa, Mafunzo yaliyofanyika katyika Ukumbi wa mikutano chumba namba sita katika Hospitali ya Wilaya Kinyonga.
Maongezi amesema Serikali imeweka utaratibu ambao mtumishi anayetaka kuacha kazi anatakiwa kuufuata.
Amesema kuna baadhi ya watumishi wamekuwa wakiacha kazi kiholela kitu ambacho muda mwingine kinaleta usumbufu kwa serikali.
“Mtu mwingine unastukia tu hayupo kituoni ukifuatilia unaambiwa kaacha kazi kapata kazi katika shirika Fulani au mwingine anaandika tu barua naacha kazi Mke wangu anaumwa sana kabla barua haijafika katika uongozi anaondoka, wakati kuna vitu vingine vinaweza kutafutiwa ufumbuzi hata bila ya kuacha kazi’ alisema maongezi
Pia amewataka watumishi kutunza siri za wagonjwa wanao wahudumia na pamoja na kutunza siri za ofisi wanazofanyia kazi.
“Idara yetu ni nyeti sana na katika majukumu yetu tunakutana na watu wenye magonjwa mbalimbali sasa sitegemei kusikia mtumishi ametoa siri za mgonjwa au siri za ofisi ni kosa kubwa sana na linaweza kukufukuzisha katika utumishi wa umma” alihitimisha Maongezi
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Kilwa Dokta Khalfanis Elekizemba amewataka watumishi kuto kukatishwa tamaa na changamoto wanazokutana nazo katika kutekeleza majukumu yao katika vituo walivyopangiwa badala yake wazitumie kama fursa kuhakikisha zinawajenga na kusonga mbele
Aidha amewataka kutumie pesa za vituo kwa kufuata utaratibu ili kuepuka hoja za kikaguzi kuhusu matumizi ya pesa hizo.
Akihitimisha mafunzo hayo Katibu wa Afya Hospitali ya Kinyonga Bi. Zabibu Uledi amewataka watumishi kutumia Lugha zenye staha wakiwa maeneo ya kazi na nje ya maeneo ya kazi pamoja na kuacha matumizi ya simu pindi wanapohudumia wagonjwa.
Aidha amewataka kutojihusisha na tabia hatarishi kama vile uesharati, ushoga, matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na ulevi uliopindukia.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa