Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wanaounda timu ya (Kurugenzi Sports Club) wamekutana na kupata iftari ya pamoja ambayo imeambatana na Matukio mbalimbali ikiwemo Mchezo wa Kirafiki baina Timu ya Watumishi kutoka Kaskazini na Timu ya Kusini, ambapo pia wamejadili kuhusu maendeleo ya Kimichezo kwa Timu ya Kurugenzi Sport Club na Watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa Ujumla.
Hayo yamefanyika Jana Tarehe 26/03/2025 kata ya Tingi katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ilulu ambapo hatua hiyo pia imekuwa moja ya maandalizi ya kushiriki Mashindano ya Mashindano ya Kimichezo ya Watumishi wa Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) ambayo kitaifa mwaka huu yatafanyika Mkoani Tanga.
Akizungumza katika Kikao Hicho Mwenyekiti wa Timu ya Kurugenzi Sport Club Mwl. Juma Mhando ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa ushirikiano wanaowapatia katika kila hatua, pia ametumia nafasi hiyo kuiomba halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kuwasaidia katika kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA kwani chachu yao kubwa ni kuhakikisha wanaacha historia nzuri ya ushindi katika Mashindao hayo.
Hata hivyo Afisa Utamaduni,sanaa na Michezo wilaya ya Kilwa Ndg. Veneranda Maro imeipongeza Timu hiyo kwa Hatua nzuri ya Kuimarisha michezo na kutengeneza uhusiano mzuri baina yao kupitia Matukio mbalimbali ikiwemo tukio hilo la Iftar,pia amewaambia watashiri Mashindano hayo hivyo amewataka kufanya Mazoezi ziadi na kujiandaa vizuri ili kuweza malengo yao ya Ushindi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa