Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Korea (KOICA), kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, limetoa mafunzo ya utalii kwa waongoza watalii katika Wilaya ya Kilwa. Mafunzo hayo yatakayo fanyika Siku 2 kuanzia Tarehe 22 hadi 23 mei 2025 yamelenga kuwaongezea ujuzi na mbinu za kisasa ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za utalii.
Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 22 Mei 2025 katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa na yamehusisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii wilayani humo, wakiwemo wanafunzi wa kada ya utalii kutoka Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa,kituo cha mawasiliano Kilwa na wadau wengineo wa utalii katika Wilaya ya Kilwa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Abushiri Mbwana, amesema kuwa mafunzo hayo ni hatua muhimu katika kuongeza fursa za ajira na kuchangia ustawi wa sekta ya utalii kwa Halmashauri hiyo na taifa kwa ujumla.
Adha amewataka wadau waliopatiwa elimu hiyo juu ya namna ya kuongeza watalii,kushirikisha jamii katika utalii, kushirikiana kwa pamoja kufikisha elimu hiyo kuhusiana na utalii katika jamii ili kufikia malengo ya mafunzo hayo.
Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo hayo, Bi. Eunice Ulomi, amewahamasisha wadau wa utalii wilayani Kilwa kuwekeza zaidi katika sekta hiyo kwa kuanzisha huduma kama makazi ya muda kwa watalii (home stay), hoteli na shughuli za utalii wa fukwe. kwani uwekezaji huo utawavutia watalii kukaa kwa muda mrefu zaidi katika eneo hilo badala ya kutafuta maeneo mbadala kwa ajili ya mapumziko.
Wanufaika wa mafunzo hayo wamelishukuru Shirika KOICA na wadau wengine kwa kuwapatia elimu itakayowawezesha kuboresha huduma wanazotoa na kuongeza ufanisi katika shughuli zao za kila siku za utalii.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa