Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed Said Magaro amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wanasimamia Ukusanyaji wa Mapato ya Vijiji na Halmashauri katika maeneo yao. Katika kutekeleza jambo hilo amewaelekeza Watendaji hao kuwa wabunifu katika kuibua vyanzo vipya vya mapato na kuendeleza vyanzo vilivyopo. Pia amewataka kuhakikisha Mapato yote yanayokusanywa yanapelekwa benki kama sheria na kanuni zinavyoelekeza.
Ndg. Magaro ameyasema hayo wakati wa Kikaokazi baina ya Timu ya Menejimemti ya Wilaya ya Kilwa (CMT), Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Watendaji wa Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kilichafayika katika Ukumbi wa Shule ya Sekeondari Kilwa tarehe 13/02/2025.
Aidha, Ndg Magaro amewataka watendaji hao kutumia mamlaka walizonazo kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata na vijiji vyao, kusimamiza matumizi bora ya ardhi, kudhibiti biashara haramu (Magendo) pamoja na usafi na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya Kata na Vijiji vyao.
Samabamba na hayo Mkurugenzi Mtendaji ametoa pongezi kwa watendaji hao kwa kusimamia vyema mazoezi ya Kitaifa ikiwemo Uchaguzi wa Viongozi wa serikali za Mtaa uliofanyika 27/Novemba/2024 na Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura uliofanyika kuanzia 28/01/2025 - 03/02/2025. Pia amehadi kufanyia kazi changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo kuhakikisha wanapata stahiki zao za uhamisho, likizo na nyinginezo ili kuwaweka katika nafasi nzuri ya kutekeleza majukumu yao.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa