Msimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo ya Kilwa Kaskazini na Kilwa Kusini, Ndg. Shija L. Lyella, tarehe 27 Agosti 2025 amewateua wagombea watatu (3) kugombea ubunge katika jimbo la Kilwa Kaskazini na wanne (4) kugombea ubunge katika jimbo la Kilwa Kusini.
Kwa upande wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, wafuatao wameteuliwa kugombea nafasi hiyo:
1. Mohamed Mshamu Ngulangwa – CUF
2. Shaweji Mohamed Mketo - ACT-Wazalendo
3. Kinjeketile Ngombare Mwiru - CCM
Kwa upande wa Jimbo la Kilwa Kusini, walioteuliwa kugombea ni:
1. Mohamedi Rashid Mahadhi – CHAUMMA
2. Abuu Mussa Mjaka – CUF
3. Hasnain Gulamabbas Dewji - CCM
4. Idrissa Abdul Kweweta - ACT Wazalendo
Msimamizi wa Uchaguzi ameeleza kuwa wagombea hao wametimiza vigezo vya kisheria vya kugombea ubunge kwa majimbo hayo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa