Kilwa,
Kuelekea maadhimisho ya siku ya maji duniani machi 22 wananchi wametakiwa kuthamini na kutunza vyanzo vya maji ili viweze kudumu kwa muda mrefu.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mhandisi wa Maji Wilaya ya Kilwa Ndg. Bady Mussa alipokua akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake mjini Kilwa masoko.
Bady amesema iwapo vyanzo vya maji vitatunzwa vitasaidia upatikanaji wa maji ya uhakika majumbani na katika taasisi mbalimbali kwa kua maji yakutosha yatapatikana kutoka katika vyanzo hivyo.
“Niwakumbushe tu wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya ambavyo vinatupatia maji kwa matumizi yetu ya kila siku, tuvitunze ili viweze kudumu vizazi na vizazi
Maji ni uhai na viumbe hai vinahitaji maji ili viishi, hivyo basi tushirikiane kwa pamoja katika suala zima la uhifadhi wa vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla” alisistiza Bady
Pia amezitaka jumuiya za maji kuhakikisha zinatekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa ili kuleta matokeo chanya katika maeneo yao.
Kaimu Mhandisi Wa Maji Wilaya ya Kilwa Ndg. Bady Mussa akisisitiza jambo alipokua kaizungumza na mwandishi wetu ofisini kakwe.
Aidha amewapongeza baadhi ya wananchi kwa kuamua kubadilika na kuacha tabia ya kuharibu miundo mbinu kwa makusudi pamoja na kuiba vifaa katika vituo vya kutolea huduma ya maji.
” Niwapongeze ndugu zangu wa kilwa kwani kwa siku za hivi karibuni hatujapokea kesi za wizi wa vifaa katika vituo vya kutolea huduma ya maji ukilinganisha na miezi kadhaa iliyopita ambapo kulikua na wimbi la wizi wa koki”.
Kila ifikapo Machi 22 Tanzania inaungana na nchi zingine ulimwenguni kuadhimisha siku ya ya Maji duniani kutokana na umuhimu wake kwa maisha ya Binadamu na viumbe hai kwa ujumla.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa