WANANCHI WA KILWA KUNUFAIKA NA UWEKEZAJI ZAO LA MIHOGO
Zao la mihogo kwa muda mref limekuwa likilimwa katika maeneo mengi hapa nchini kwa ajili ya matumizi ya chakula, mihogo ni zao ambalo linalimwa karibu mikoa yote hapa nchini.
Kwa siku za hivi karibuni wananchi wameanza kusikia uwekezaji mkubwa katika baadhi ya mikoa kama Tanga na Pwani ambapo zao hili sasa linalimwa na kusindikwa viwandani na kisha kusafirishwa kama malighafi kwenda barani Asia hasa nchini China.
Wilaya ya Kilwa ni kati ya Wilaya chache hapa nchini yenye ardhi kubwa na yenye rutuba inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi ya biashara na chakula. Kwa muda mrefu wakazi wa Wilaya ya Kilwa kama ilivyo maeneo mengine ya ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi walikuwa wanategemea zao la Korosho kama zao kuu la biashara na baadaye kwa miaka ya hivi karibuni zao la ufuta likaongezeka na kufanya kuwa na mazao makuu mawili ya biashara.
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wa Wilaya ya Kilwa ndg John Mkinga anasema Wilaya hiyo ina eneo la hekta za mraba laki nane na themanini elfu(880,000) linalofaa kwa kilimo cha mazao mbali mbali huku mpaka sasa eneo lililolimwa Hekta za mraba themanini elf utu(80,000) na maeneo mengine yaliyobaki yakiendelea kuwa mapori.
Serikali ya awamu ya tano inayoogozwa na Mhe.Dr.John Pombe Magufuli tangu iingie madarakani imekuwa ikisisitiza uchumi wa viwanda na uzalishaji wa mazao yenye tija, Hali hiyo imepelekea serikali ya Tanzania na serikali ya China kusaini mkataba wa uzalishaj na safirishaji wa zao la Mihogo kutoka nchini Tanzania kwenda nchini china ambapo Zaidi ya tani milioni tano zinahitajika kila mwaka.
Mwenyekiti wa makampuni ya PAM AFRICAN DEVELOPMENT LIMITED Bi.Dior Feng alifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi akiwa na ujumbe wake kujitambilisha kwa Mkuu wa Mkoa Mhe.Godfrey Zambi lengo likiwa ni kutafuta maeneo ya uwekezaji katika mkoa huo. Tarehe 24Septemba 2019 Mkuu wa Mkoa na ujumbe wake aliongozana na wawekezaji hao kufika katika Wilaya ya Kilwa kuona utayari wa wananchi katika kuukarbisha uwekezaji huo wenye thamani kubwa. Mhe.Zambi katika kikao chake cha Kwanza katika kijiji cha Mavuji kata ya Mandawa aliwatambulisha wawekezaji hao ambapo wananchi walionesha furaha kubwa na kuwakaribisha wawekezaji hao kuja kuwekeza katika maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.Christopher Ngubiagai aliyeambatana na mkuu wa Mkoa katika ziara hiyo alitaja baadhi ya faida ya wekezaji huo kuwa ni ajira kwa wakazi wa maeneo hayo, soko la bidhaa zao pamoja upatikanaji wa huduma za kijamii kama maji na Afya katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg.Renatus Mchau alimthibitishia Mkuu wa Mkoa mbele ya wananchi hao kuwa ofisi yake ilishafanya maandalizi ya awali katika vijiji vitakavyohusika katika awamu ya kwanza ya uwekezaji huo ambapo wananchi wote walionesha kuupokea mradi huo. Mkurugenzi alitaja vijiji vitakavyohusika katika awamu ya kwanza kuwa ni Mavuji, Naenokwe,Liwiti na Migelegele ambapo katika awamu hiyo ya kwanza jumla ya hekta elfu arobaini (40,000) itatumika kwa kilimo na ujenzi wa viwanda vya usindikaji.
Mkugenzi pia aliwaeleza wananchi hao kuwa pamoja na wawekezaji hao kupewa eneo la kulima lakini bado mahitaji yao ni makubwa Zaidi na hivyo kuwataka wanchi hao kuanza kufikiria maanadalizi ya mashamba makubwa na Mihogo kwani waweekezaji hao watanunua pia Mihogo kutoka kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa alihitimisha ziara yake katika kijiji cha Migelegele ambapo pia wananchi walionesha furaha kubwa ya kuwapokea wawekezaj hao.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa