Wananchi na watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la vipimo na chanjo ya Homa ya Ini (Hepatitis B) lililoanza leo, tarehe 25 Agosti 2025, katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Zoezi hilo ambalo litadumu kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia tarehe 25 Agosti hadi 25 Septemba 2025, limeleta mwitikio chanya kutoka kwa wananchi na watumishi waliopata nafasi ya kujitokeza kupata huduma hiyo muhimu.
Mbali na chanjo, washiriki wamepatiwa elimu juu ya namna ugonjwa wa Homa ya Ini unavyoweza kuambukizwa na njia bora za kujikinga, hatua iliyoongeza uelewa na kuhamasisha jamii kuchukua tahadhari za kujilinda kiafya.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa