Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa kwa kushirikiana na Watumishi wa Benki ya NMB wamefanya kikao cha kujadili mikakati na elimu ya namna ya uboreshaji wa maendeleo katika wilaya hiyo.
Wakizungumzia mikakati hiyo baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo ambayo ni pamoja na kuondoa tozo katika akaunti za vijiji,shule,zahanati pamoja na vituo vingine vya kutolea huduma za kijamii, kutoa hamasa hususani kwa wakulima na wafugaji kufungua akaunti za benki pia kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi kutoa misaada kwa maeneo yenye uhitaji ikiwemo madawati,vitanda pamoja na mahitaji mengine.
Aidha, Meneja wa Benki ya NMB tawi la Kilwa Eya Ngollo amesema kuwa wao wako tayari kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi kama wadau wa Taasisi hiyo endapo tu hatua stahiki zitafuatwa kikamilifu ikiwemo barua ya maombi ambayo imeainisha maeneo yenye uhitaji zaidi wa misaada hiyo
Pia, wao kama benki wamefanya jitihada za kutoa elimu kwa wananchi hususani wa vijijini kuhusu kufungua akaunti za benki na tayari baadhi ya wananchi wamefikiwa na watumishi wao kwa kuweka kambi katika vijiji husika
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa