Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo amewataka wataalamu wa Kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kutoa Elimu kwa wakulima ili waweze kuachana na utaratibu wa Kilimo cha Kuhamahama ambacho kinapelekea kuongezeka kwa vitendo vya uharibufu wa mazingira unavyotokana na ukataji wa miti katika uandaaji wa mashamba.
Hayo ameyasema leo Tarehe 17/03/2025 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Wiki ya Upandaji Miti iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Dodomezi iliyoko Katika Kata ya Kivinje Wilayani kilwa. Kampeni hiyo imepambwa na Kauli mbiu isemayo “MTI WANGU, MPAKA WANGU, TUHIFADHI MAZINGIRA’’
Sambamba na hayo Mhe. Nyundo amewata mwanafunzi wote katika Shule zote za Wilaya ya Kilwa kuhakikisha wanapanda Miti na kuitunza vizuri ili kusaidia kupata miti ya Matunda. Upatikanaji wa matunda mashuleni utasaidia kuimarisha Afya za wanafunzi, lakini pia kuongeza kasi ya upandaji Miti katika Wilaya ya Kilwa
Kwa upabde wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed Magaro amewataka wanafunzi na wananchi Wilayani ya Kilwa kuwa na desturi ya upandaji miti katika Mazingira yao ya nyumbani ili kupunguza Athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi yanayopelekea kuongezeka kwa Joto na kukosekana kwa mvua katika mtiririko maalumu.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa