Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilwa Ndg. Said Ally Timamy amewatakata wajumbe Halmashauri Kuu ya Chama hicho kuipongeza Serikali ya Awamu sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa utoaji wa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo Wilayani Kilwa. Ameyaeleza hayo wakati wa kikao cha uwasilishaji na upokeaji wa Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2024 kilichofanyika Ukumbi wa Sultani Kilwa Masoko tarehe 26/02/2025.
Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo, amewaomba wajumbe wa Halmashauri kuu kushirikiana na watumishi wa Halmashauri pamoja na Taasisi zilizopo katika wilaya ya Kilwa, kuhakikisha wanatekeleza miradi ya Maendeleo kwaajiri ya wananchi wa wilaya hiyo. Aidha ameeleza kuwa Serikali kupitia Wakala wa Usamabazaji wa Maji na USafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imejipanga kuhakikisha vijiji vyote 90 vya Wilaya ya Kilwa vinapata huduma ya maji safi na Salama, Aidha ameeleza mpango wa serikali kupitia Wakala wa Barabara wa Vijijini na Mijini (TARURA) wa kuboresha maeneo yenye changamoto ya mtandao wa barabara hususani kwa Kata ya Kandawale na Kibata.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini Mhe. Ally Kasinge amesema tayari serikali imehidhinisha fedha kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji katika kata za Pande na Lihimalyao Hii ni moja ya kuhakikisha vijiji 90 vya Halmashauri ya Kilwa vinapata huduma ya Maji safi na salama. Sambamba na hayo Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini Mhe. Francis Ndulane ameeleza kuwa Serikali inatambua changamoto ya usafiri Wilayani Kilwa na imeshaanza mchakato wa utengenezaji wa barabara na madaraja yaliyoathirika na Kimbunga hidaya.
Aidha Ndg. Timamy amewataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi kama inavyotakiwa ili kuhakikisha wanatimiza ahadi zilizotolewa kwa wananchi na kuendelea kutengeneza imani ya Chama cha Mapinduzi Wilayani kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa