Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe. Charles Kazungu ameongoza mafunzo juu ya ukusanyaji wa mapato yatokanayo na chanzo cha madini kwa Wahe. Madiwani, Wabunge na Wataalam kutoka Katika Halmashauri za Kilwa na Nsimbo. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita tarehe 17/12/2024.
Katika mafunzo hayo Mhe. Kazungu amesisitiza umuhimu wa Wanasiasa kushirikiana na watendaji katika Halmashauri kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanakusanywa kikamilifu. "Ili kufanikiwa katika ukusanyaji wa mapato ni muhimu sana Wahe. Madiwani kushirikiana na wataalamu katika opereseheni za ukusanyaji wa mapato, Kwa hapa kwetu Geita Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango wanakuwa msitari wa mbele pamoja na wataalam kuhakikisha mapato yanakusanywa" amesema Mhe. Kazungu
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe. Rashid Msaka kwa niaba ya Wahe. Madiwani, Wabunge na wataalam kutoka Wilayani Kilwa ametoa salamu za Shukrani kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kuandaa mafunzo mazuri yenye maarifa ya kutosha yatakayowezesha ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa